China na Ufaransa zinapaswa kuimarisha uratibu wa kimkakati na ushirikiano: Waziri wa Mambo ya Nje wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 22, 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mjini Paris, Ufaransa, Februari 20, 2024. (Ikulu ya rais wa Ufaransa/ Xinhua)

PARIS - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi kwenye mkutano wake na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Paris siku ya Jumanne amesema kuwa China na Ufaransa zinapaswa kuimarisha uratibu wa kimkakati na kuongeza ushirikiano ili kutoa mchango kwa ajili ya amani na utulivu duniani.

Wang ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amewasilisha salamu za Rais Xi Jinping wa China kwa Macron, akisema kuwa wakuu hao wawili wameanzisha hali thabiti ya kuaminiana na urafiki wa dhati, na kuongoza maendeleo ya ushirikiano wa kimkakati wa pande mbili, wakitoa ushawishi mkubwa na chanya kwa Dunia.

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa, ikiwa inatoa hatua muhimu ya kujenga kutoka kwenye mafanikio yaliyopita na kusonga mbele, Wang amesema, akiongeza kuwa pande zote mbili zinapaswa kuchukulia maadhimisho hayo kama fursa ya kufanya majumuisho ya safari ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, kuenea uzoefu muhimu na hatua zenye mafanikio, na kupanga kwa pamoja miaka 60 ijayo ya uhusiano kati ya China na Ufaransa.

Wang amesema China inapenda kushirikiana na Ufaransa kushikilia matarajio ya awali, kuendelea kuweka umakini, kuimarisha ushirikiano na kufungua siku zijazo.

Wang pia ameeleza matumaini yake kuwa Ufaransa itaweka mazingira ya haki na usawa ya biashara na kutoa matarajio mazuri na thabiti ya muda mrefu kwa kampuni za China nchini Ufaransa.

Kwa upande wake Macron amemtaka Wang kufikisha salamu zake za dhati kwa Rais Xi na kuwatakia Wachina kila la heri katika Mwaka wa Dragoni.

Akikumbuka kwa furaha ziara yake ya mwaka jana nchini China yenye mafanikio, Macron amesema anatarajia kushirikiana na China kufanya maandalizi ya mawasiliano ya ngazi ya juu mwaka huu, na anatumai kuwa pande hizo mbili zitatumia fursa ya Mazungumzo ya Kimkakati kati ya Ufaransa na China kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na yeye na Rais Xi, na kujenga zaidi uhusiano wa kudumu na wa karibu kati ya Ufaransa na China.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mjini Paris, Ufaransa, Februari 20, 2024. (Ikulu ya rais wa Ufaransa/ Xinhua)

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), mjini Paris, Ufaransa, Februari 20, 2024. (Ikulu ya rais wa Ufaransa/ Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha