Benki ya Dunia yazipatia Zambia na Tanzania dola milioni 270 ili kuboresha uchukuzi na muunganisho wa biashara

(CRI Online) Februari 22, 2024

Benki ya Dunia imezipa Zambia na Tanzania ruzuku ya dola za Kimarekani milioni 270 kusaidia kuboresha uchukuzi na biashara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano, fedha hizo zinakusudiwa kuboresha usafirishaji na mabadilishano ya biashara kwenye ukanda wa Dar es Salaam kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni sehemu ya mradi wa miaka sita wa Ukanda wa Usafiri wa Kuhimili Uchumi, unaolenga kuongeza ufanisi, muuganisho na uhimilivu wa tabianchi katika usafirishaji muhimu wa kikanda na njia za biashara za mashariki na kusini mwa Afrika.

Meneja wa Benki ya Dunia nchini Zambia, Achim Fock, amesema katika taarifa yake kwamba mradi huo ni dhamira kubwa ya biashara na usafirishaji wa kikanda, na kuongeza kuwa sekta za usafirishaji na ugavi zinatarajiwa kupata msukumo kutokana na shughuli husika zinazolenga kujenga uwezo wa kitaasisi na kisekta.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mradi huo utawanufaisha watu 2,500,000 nchini Zambia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha