China yashuhudia ongezeko kubwa la matumizi ya manunuzi wakati wa Likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 23, 2024

Picha iliyopigwa Februari 5, 2024 ikionyesha mandhari ya gulio la Mwaka Mpya wa Jadi wa China karibu na Mto Manjano huko Lanzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Gansu, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Ma Xiping)

Picha iliyopigwa Februari 5, 2024 ikionyesha mandhari ya gulio la Mwaka Mpya wa Jadi wa China karibu na Mto Manjano huko Lanzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Gansu, Kaskazini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Ma Xiping)

Beijing - China imeshuhudia ongezeko kubwa la matumizi ya manunuzi wakati wa Likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ikiashiria mwanzo mzuri wa Mwaka 2024, He Yadong msemaji wa Wizara ya Biashara ya China amesema Alhamisi.

He amesema kuna maeneo mengi yaliyofanya vema katika matumizi ya manunuzi ya bidhaa wakati wa likizo. Ameelezea takwimu za kampuni za kuuza bidhaa za reja reja zinazofuatiliwa na wizara hiyo, ambapo mauzo ya bidhaa za dhahabu, fedha na vito yameongezeka kwa asilimia 23.8, mauzo ya bidhaa za michezo na burudani yameongezeka kwa asilimia 15.6, na yale ya vifaa vya mawasiliano yameongezeka kwa asilimia 10.4.

Matumizi ya manunuzi katika sekta za huduma za China yameshuhudia ukuaji mkubwa katika kipindi hicho. Watalii wa ndani wametumia yuan bilioni 632.69 (kama dola bilioni 89 za Kimarekani), ikiwa ni ongezeko la asilimia 47.3 mwaka hadi mwaka, wakati thamani ya mauzo ya tiketi za filamu katika sinema kote nchini ilifikia yuan bilioni 8.02 katika kipindi cha mwaka mpya wa jadi wa China, amesema.

Msukumo wa matumizi mapya ya manunuzi pia umejitokeza. Mauzo ya rejareja ya papo hapo kupitia majukwaa ya biashara ya mtandaoni yaliyofuatiliwa na wizara hiyo yalipanda kwa asilimia 32.2 mwaka hadi mwaka, na baadhi ya majukwaa yameshuhudia mauzo ya vifaa vya baiskeli na kuteleza kwenye barafu yakiongezeka kwa asilimia zaidi ya 50 kutoka mwaka uliopita, amesema.

Wizara hiyo itapanga mfululizo wa shughuli za kuhamasisha matumizi ya manunuzi na kutekeleza kikamilifu hatua za kupanua matumizi ya manunuzi, amesema He, huku akitabiri kuwa soko la watumiaji wa manunuzi litaongezeka kwa kasi katika robo ya kwanza ya Mwaka 2024. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha