Pato la Kiuchumi la Beijing-Tianjin-Hebei laongezeka kwa asilimia 90 katika muongo mmoja uliopita

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 23, 2024

Watu wakitembelea kituo cha maonyesho cha Eneo Huria la Kitaifa la Kielelezo cha Uvumbuzi la Zhongguancun mjini Beijing, China, Mei 27, 2023. (Xinhua/Zhang Chenlin)

Watu wakitembelea kituo cha maonyesho cha Eneo Huria la Kitaifa la Kielelezo cha Uvumbuzi la Zhongguancun mjini Beijing, China, Mei 27, 2023. (Xinhua/Zhang Chenlin)

BEIJING - Eneo la Beijing-Tianjin-Hebei nchini China limeshuhudia pato lake la kiuchumi (GDP) likikua kwa asilimia 90 hadi kufikia yuan trilioni 10.4 (kama dola trilioni 1.46 za Kimarekani) Mwaka 2023 ikilinganishwa na kiwango cha 2013, takwimu zilizotolewa Alhamisi zinaonyesha.

Katika kuondoa majukumu yake yasiyohusiana na hadhi yake ya kuwa mji mkuu wa China, Beijing imefunga viwanda vya kampuni zaidi ya 3,000 na kufunga au kuboresha masoko na vituo vya usafirishaji na uchukuzi wa bidhaa zaidi ya 1,000 katika muongo mmoja uliopita, Liu Bozheng, Naibu Mkurugenzi wa ofisi ya Beijing inayosimamia ujumuishaji wa Eneo la Beijing-Tianjin-Hebei, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari Alhamisi.

Katika ishara ya ukuaji wa kiwango cha juu, idadi ya mashirika mapya ya biashara mjini humo katika viwanda vya uzalishaji bidhaa za gharama ya juu za teknolojia, biashara, utamaduni na upashanaji wa habari kati ya yote imeongezeka hadi asilimia 66.1 Mwaka 2023 kutoka asilimia 40.7 Mwaka 2013, afisa huyo amesema.

Katika muongo mmoja uliopita, kampuni kutoka Zhongguancun, eneo la kitaifa la maendeleo ya viwanda vya teknolojia ya hali ya juu la Beijing, zilianzisha matawi zaidi ya 10,000 huko Tianjin na mkoani Hebei.

Wakati huo huo, kampuni za Beijing zilifanya uwekezaji wa biashara au miradi 49,000 katika sehemu mbili jirani wenye thamani ya jumla ya yuan trilioni 2.3.

Kadiri ujumuishaji unavyoendelezwa kwa kasi, eneo hilo limejenga reli na barabara kuu zaidi ili kuimarisha mafungamano.

Eneo la Beijing-Tianjin-Hebei lina njia za reli zenye urefu wa kilomita zaidi ya 11,000, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 30 kutoka Mwaka 2013, na barabara kuu zenye urefu wa karibu kilomita 11,000, sawa na ongezeko la asilimia 40 kutoka Mwaka 2013, takwimu zinaonyesha. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha