Kusimamishwa kwa mapigano mara moja huko Gaza ni jambo la haraka kwa sasa: Mjumbe wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 23, 2024

Watu wakiwa katika eneo linaloteketezwa kwenye shambulizi la anga la Israel katika Mji wa Rafah, Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 22, 2024. (Picha na Yasser Qudih/Xinhua)

Watu wakiwa katika eneo linaloteketezwa kwenye shambulizi la anga la Israel katika Mji wa Rafah, Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 22, 2024. (Picha na Yasser Qudih/Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa balozi Zhang Jun amesema siku ya Alhamisi kwamba kusimamisha vita mara moja huko Gaza ni jambo la haraka kwa sasa na kwamba asili ya hatua yoyote ya Baraza la Usalama ni kufikia usimamishaji wa mapigano mara moja. Akisema kuwa kura ya hapana ya Marekani dhidi ya azimio lililoandaliwa na Algeria Jumanne ilimaanisha kuwa Baraza hilo limekosa fursa nyingine ya kuhimiza usimamishaji vita huko Gaza.

Kuendelea kwa mgogoro huo hata kwa siku moja nyingine kunasababisha vifo vingi zaidi vya raia na maafa makubwa zaidi. Kusimamishwa kwa mapigano mara moja huko Gaza ni jambo la haraka ili kuokoa maisha ya watu wasio na hatia na kuzuia kuenea kwa vita, Balozi Zhang amesema.

"Kusimamishwa kwa mapigano mara moja ni matarajio ya pamoja yaliyotolewa na jumuiya ya kimataifa na makubaliano ya idadi kubwa ya nchi wajumbe wa Baraza la Usalama," ameliambia Baraza la Usalama.

Zhang amesema China inafahamu kuwa Marekani imewasilisha rasimu yake ya azimio, na inatumai kuwa Marekani itaonyesha msimamo wake wa kuwajibika, kuitikia wito wa kimataifa, na kuheshimu maelewano kati ya nchi wajumbe wa Baraza la Usalama,.

Amesema watu zaidi milioni 1.5 wa Gaza wamejazana mjini Rafah, wakiwa hawana mahali pengine pa kwenda na kwamba uvamizi wa kijeshi wa Israel huko Rafah utasababisha vifo vya raia na maafa ya kibinadamu na kuleta uharibifu usioweza kurekebishwa kwa amani ya eneo hilo.

"China inapinga vikali vitendo hivyo. Israel inapaswa kufuta mara moja mipango yake ya kushambulia Rafah na kusitisha adhabu yake ya jumla kwa watu wa Palestina. Amri ya hatua za muda zinazolenga kuzuia mauaji ya halaiki ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki lazima itekelezwe ipasavyo bila kuchelewa” amesema.

Amesema, makosa ya kihistoria yanayowakumba watu wa Palestina lazima yarekebishwe. Matarajio ya Palestina ya kuanzisha taifa huru lazima yatimizwe.

Watu wakionekana katika jengo lililobomolewa baada ya shambulizi la anga la Israel katika Mji wa Rafah, Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 22, 2024. (Picha na Yasser Qudih/Xinhua)

Watu wakionekana katika jengo lililobomolewa baada ya shambulizi la anga la Israel katika Mji wa Rafah, Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Februari 22, 2024. (Picha na Yasser Qudih/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha