Hospitali za China na Sierra Leone zatia saini makubaliano ili kuimarisha ushirikiano wa kimatibabu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 23, 2024

Daktari wa China akimchunguza mgonjwa katika Hospitali ya Urafiki kati ya Sierra Leone na China huko Jui, mji ulio katika kitongoji cha Freetown, Sierra Leone, Februari 22, 2024. (Xinhua/Shi Yu)

Daktari wa China akimchunguza mgonjwa katika Hospitali ya Urafiki kati ya Sierra Leone na China huko Jui, mji ulio katika kitongoji cha Freetown, Sierra Leone, Februari 22, 2024. (Xinhua/Shi Yu)

FREETOWN - Hospitali ya Tatu ya Xiangya ya Chuo Kikuu cha Kusini ya Kati cha China imetia saini makubaliano na Hospitali ya Urafiki kati ya Sierra Leone na China siku ya Alhamisi ili kuimarisha ushirikiano wa matibabu kati ya nchi hizo mbili katika mji mdogo wa Jui, ulio katika kitongoji cha Mji wa Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone.

Chini ya makubaliano hayo, hospitali hiyo ya China ambayo ni moja ya hospitali za kiwango cha juu katika Mkoa wa Hunan katikati mwa China, itatoa msaada zaidi wa matibabu kwa mwenzake, haswa katika uuguzi.

Kwa mujibu wa Yan Jin, mkurugenzi wa idara ya wauguzi ya hospitali hiyo ya China, hospitali hiyo inafanya ushirikiano wa miongo kadhaa na wenzao wa Afrika kwa kupeleka wafanyakazi karibu 20 wa matibabu katika bara hilo.

Hospitali hiyo ya China inapenda kupokea wahudumu wanaozuru kutoka hospitali ya Sierra Leone kwa mafunzo ya matibabu katika maeneo maalum, kama vile usimamizi wa kitengo cha huduma maalum kwa mtoto, Yan amesema katika hafla ya kutia saini.

Sarah Conth, Mkuu wa Hospitali ya Urafiki kati ya Sierra Leone na China, amebainisha kuwa kitengo cha huduma maalum kwa watoto katika hospitali yake kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kulisha watoto na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya. Ametoa shukrani zake kwa China kutokana na msaada wake wa muda mrefu kwa hospitali hiyo katika kuboresha ufanisi wake.

Hospitali ya Urafiki kati ya Sierra Leone na China, ambapo timu za matibabu za China zinafanya kazi, ni moja ya hospitali kubwa zaidi nchini Sierra Leone. 

Wawakilishi wakihudhuria hafla ya kutia saini katika Hospitali ya Urafiki kati ya Sierra Leone na China huko Jui, mji ulio katika kitongoji cha Mji wa Freetown, Sierra Leone, Februari 22, 2024. (Xinhua/Shi Yu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha