Maeneo kame ya Kenya yakabiliwa na maradhi kutokana na mvua za El Nino

(CRI Online) Februari 23, 2024

Maeneo kame na nusu kame ya Kenya sasa yako katika jitihida za kukabiliana na athari zinazotokana na mvua za El Nino baada ya kukumbwa na ukame mkali zaidi katika miongo kadhaa iliyopita.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi na Mamlaka ya Taifa ya Kukabiliana na Ukame ya Kenya (NDMA) inasema maeneo yote 23 ya nchi hiyo yanayochukuliwa kama sehemu kame na nusu kame hayana hali ya ukame. Lakini zimeibuka hatari zinazohusiana na ongezeko la mvua, ikiwa ni pamoja na mlipuko wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF), hali ambayo inaathiri mifugo katika maeneo ambayo ufugaji ndiyo tegemeo.

Kwa mujibu wa Kamati ya Usimamizi wa El Nino ya Kenya, Kenya ilikumbwa na mvua za El Nino kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka 2023, hali ambayo iliathiri zaidi maeneo kame na nusu kame, na kusababisha vifo vya watu takriban 120, uharibifu wa mali, na maelfu ya watu kupoteza makazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha