Xi ajibu barua kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Muscatine ya Marekani

(CRI Online) Februari 26, 2024

Rais Xi Jinping wa China siku ya Jumamosi ambayo pia ni sikukuu ya taa ya Mwaka wa Jadi wa Dragoni wa China, alijibu barua kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Muscatine iliyopo katika Jimbo la Iowa, Marekani ambao walitembelea China mwishoni mwa Januari.

Kwenye barua yake, Rais Xi amewahimiza wanafunzi wa shule hiyo kutembelea tena China na kuwakaribisha vijana zaidi wa Marekani kuja China ili waweze kuiona China halisi, kujenga urafiki halisi na vijana wa China, na kutoa mchango wao katika kuimarisha urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha