Soko la simu janja za kukunjika la China lashuhudia kupanuka Mwaka 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 26, 2024

Watu wakijaribu simu za kukunjika kwenye banda la kampuni ya Honor ya China kwenye maobyesho ya IFA 2023 mjini Berlin, mji mkuu wa Ujerumani, Septemba 1, 2023. (Xinhua/Ren Pengfei)

Watu wakijaribu simu za kukunjika kwenye banda la kampuni ya Honor ya China kwenye maobyesho ya IFA 2023 mjini Berlin, mji mkuu wa Ujerumani, Septemba 1, 2023. (Xinhua/Ren Pengfei)

BEIJING - Uuzaji wa simu janja za kukunjika katika soko la China uliongezeka kwa asilimia 114.5 Mwaka 2023 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia wa 2022, ripoti ya sekta hiyo imeonyesha ambapo kiasi cha uuzaji wa simu hizo kilizidi milioni saba mwaka jana, ikiashiria ongezeko la mwaka hadi mwaka la zaidi ya asilimia 100 kwa miaka minne mfululizo.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kimataifa la International Data Corporation linalojihusisha na utafiti wa soko la kimataifa ambalo limetoa takwimu hizo, ukuaji huo wa soko unachangiwa na kuboreshwa kwa uzoefu wa watumiaji na kushuka zaidi kwa bei.

Mwaka 2023, simu janja za kukunjika zilizogharimu dola 1,000 za Marekani au zaidi zilichukua asilimia 66.5 ya soko, kutoka asilimia 81 iliyorekodiwa Mwaka 2022.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha