Sherehe kwenye hekalu zafanyika Mkoa wa Henan katikati ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 26, 2024
Sherehe kwenye hekalu zafanyika Mkoa wa Henan katikati ya China
Wasanii wa kijadi wakicheza ngoma ya simba kwenye sherehe zilizofanyika katika hekalu katika wilaya ya Xunxian, Mkoa wa Henan katikati ya China, Februari 25, 2024.

Wakazi wa huko wa kundi la maonesho ya Shehuo wameshiriki katika sherehe kwenye hekalu huko Xunxian siku ya Jumapili, siku moja baada ya Sikukuu ya Taa za jadi ya China. Shehuo ni sherehe ya kijadi yenye kufanana na kanivali, ambapo watu wanafanya maonyesho ya kucheza ngoma ya dragoni, ngoma ya simba, kufanya maonesho ya opera ya kijadi ya China, kupiga ngoma na kufanya maonyesho mengine ya kitamaduni ambayo ni ya aina mbalimbali tofauti katika maeneo tofauti. (Picha na Zhang Tingyuan/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha