China yatoa wito wa suluhu ya kisiasa kwenye mgogoro wa Ukraine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 26, 2024

Zhang Jun (Kati, Mbele), mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa (UN), akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu mgogoro wa Ukraine, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Februari 23, 2024. (Xinhua/Xie E )

Zhang Jun (Kati, Mbele), mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa (UN), akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu mgogoro wa Ukraine, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Februari 23, 2024. (Xinhua/Xie E )

UMOJA WA MATAIFA - Zhang Jun, Mjumbe wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa (UN) siku ya Ijumaa alitoa wito wa kufanyika juhudi za kimataifa katika kutatua mgogoro wa Ukraine akisema kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya juhudi kwa pamoja kutafuta suluhu ya haki na halali ili mgogoro huo uweze kutatuliwa kisiasa na amani itawale.

Ametoa wito huo kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliopangwa kuambatana na kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu kuanza kwa operesheni maalum ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine.

Mgogoro wa Ukraine umesababisha uharibifu usioweza kuhesabika. Hatua ya dharura zaidi ni kusimamisha mapigano, kuanzisha mazungumzo ya amani na kurejesha amani. Amani ni kwa maslahi ya pande zote, amesema Zhang.

China inatoa wito kwa pande husika kuonyesha hisia ya kuwajibika na kufanya juhudi za kidiplomasia za kiujenzi ili kuhimiza kupunguza uchochezi wa mgogoro na kuweka mazingira mazuri ya kuanza tena mazungumzo. Amesisitiza kuwa kuimarisha au kupanua kambi ya kijeshi hakuwezi kuhakikisha usalama wa kikanda.

"Lazima ifahamike kwamba hali ambayo Ulaya inakabiliana nayo leo inahusiana kwa karibu na upanuzi wa mara kwa mara wa NATO (Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi) kuelekea upande wa mashariki tangu mwisho wa Vita Baridi. Tunahimiza NATO kujiuliza maswali ya msingi, kutoka nje ya ngome ya mawazo ya Vita Baridi na kuepuka kujifanya kama wakala wa matatizo ambayo yanachochea mapambano ya kambi. Tunamsihi mkuu wa NATO kutazama Dunia kupitia lenzi yenye muono sahihi, kuacha kuropoka vitishio na kufanya kile ambacho hakika kinafaa kwa amani ya Dunia," amesema.

Amesema, kwa kutumia mgogoro wa Ukraine kama kisingizio, baadhi ya nchi zimeweka kiholela vikwazo vya upande mmoja na mamlaka ya kutumia mkono mrefu na zimetoa shinikizo lisilo na msingi kwa biashara za nchi nyingine, na kuathiri vibaya minyororo ya viwanda na usambazaji wa bidhaa duniani na kuvuruga utaratibu wa biashara duniani.

China inapinga vikali Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya kuweka vikwazo visivyo halali dhidi ya kampuni za China kwa kutumia suala la Ukraine kama kisingizio.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha