

Lugha Nyingine
Kenya yazindua mkakati wa kukabiliana na UKIMWI, mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia
Wizara ya Afya ya Kenya imezindua mkakati wa kuondoa matishio matatu ya UKIMWI, mimba za utotoni na unyanyasaji wa kijinsia ambayo yamerudisha nyuma maendeleo ya kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030.
Waziri wa afya wa Kenya Bibi Susan Nakhumicha amesema Kenya ina watu milioni 1.5 wanaoishi na UKIMWI na asilimia zaidi ya 90 ya waathirika hao wanatumia dawa za kuokoa maisha. Amelalamika juu ya uwepo wa kiwango cha juu cha maambukizi kati ya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24.
Bibi Nakhumicha amesisitiza dhamira ya serikali ya kukomesha UKIMWI ifikapo mwaka 2030 kwa kuzuia maambukizi mapya, miongoni mwa watu walio katika hatari kubwa kama vile vijana na wanawake, sambamba na kupanua upatikanaji wa matibabu ya kurefusha maisha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma