ECOWAS yaziondolea vikwazo Burkina Faso, Mali, Niger

(CRI Online) Februari 26, 2024

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imetangaza kuondoa vikwazo vilivyoweka dhidi ya Burkina Faso, Mali na Niger vilivyokuwa na lengo la kushinikiza watawala wa kijeshi katika nchi hizo kurejea katika utaratibu wa kikatiba.

Ofisa mwandamizi wa kamisheni ya ECOWAS Bw. Omar Touray, amesema katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano maalum wa jumuiya hiyo uliofanyika mjini Abuja, kuwa vikwazo hivyo vinaondolewa mara moja.

Amesema ECOWAS pia imesema haikupokea ombi lolote kutoka kwa nchi hizo kutaka kujitoa kwenye jumuiya hiyo, na kwamba vikwazo pia vimeondolewa kwa raia wa Mali kuchaguliwa kwenye nafasi za kiuongozi katika jumuiya hiyo, na kwa serikali ya Guinea.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha