Mjumbe Maalum wa Rais wa China ashiriki kwenye mazishi ya kitaifa ya marehemu rais wa Namibia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2024

Rais mpya wa Namibia Nangolo Mbumba (wa kwanza kulia) akikutana na mjumbe maalum wa Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la  China Jiang Zuojun (wa pili kulia) katika Ikulu ya Rais huko Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Februari 25, 2024. (Xinhua/Chen Cheng)

WINDHOEK - Mjumbe Maalum wa Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China Jiang Zuojun ameshiriki kwenye mazishi ya kitaifa ya Rais wa Namibia Marehemu Hage Geingob, yaliyofanyika Windhoek, mji mkuu wa Namibia, kuanzia Jumamosi hadi Jumapili na kutoa hotuba katika hafla ya maombolezo.

Rais mpya wa Namibia Nangolo Mbumba alikutana na Jiang katika Ikulu ya Rais siku ya Jumapili mchana. Katika mkutano huo, Jiang aliwasilisha salamu za kirafiki na za kutakia kheri za Rais Xi kwa Rais Mbumba, akitoa salamu za dhati za rambirambi kwa kifo cha Rais Geingob na kutoa pole kwa serikali na watu wa Namibia.

China na Namibia zinafurahia urafiki wa jadi, na ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali umedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo katika miaka ya hivi karibuni, amesema mjumbe huyo maalum wa China.

China inatilia maanani sana uhusiano wake na Namibia na ingependa kushirikiana na serikali mpya ya Namibia katika kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa na ushirikiano wa kirafiki na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Mbumba amemshukuru Rais Xi kwa kumteua mjumbe maalum wa kutoa salamu za rambirambi na kumwomba Jiang kumfikishia salamu za dhati Rais Xi.

Amesisitiza kuwa Namibia ingependa kufanya juhudi za pamoja na China katika kuendeleza urafiki wa pande mbili na kuimarisha ushirikiano katika biashara, uwekezaji, kilimo, sayansi na teknolojia ili kuleta manufaa kwa nchi zote mbili na watu wake. 

Mjumbe Maalum wa Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni  Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China Jiang Zuojun akishiriki kwenye  mazishi ya kitaifa ya Rais wa Namibia Marehemu Hage Geingob na kutoa hotuba kwenye hafla ya maombolezo huko Windhoek, mji mkuu wa Namibia. Februari 24, 2024. (Xinhua/Chen Cheng)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha