China kutoa huduma bora kwa wawekezaji wa kigeni: Naibu Waziri Mkuu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2024

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Sukanto Tanoto,  Meneja mkuu wa Kundi la Royal Golden Eagle (RGE) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Februari 26, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Sukanto Tanoto, mwenyekiti wa Kundi la Royal Golden Eagle (RGE) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Februari 26, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

Beijing - China itaendelea kutoa huduma bora kwa wawekezaji wa kigeni, Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng amesema mjini Beijing siku ya Jumatatu kwenye mkutano na Sukanto Tanoto, mwenyekiti wa Kundi la Kampuni za Royal Golden Eagle (RGE) la Singapore, wakati pande hizo mbili zilipobadilishana mawazo juu ya maendeleo ya uchumi ya China, kuendeleza mageuzi kwa kina na kufungua mlango, na maendeleo ya biashara za kampuni za kigeni nchini China.

He ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema ufufukaji wa uchumi wa China unaendelea kwa mwelekeo mzuri, na ujenzi wa muundo mpya wa maendeleo unafanika kwa kasi, hali ambayo inatoa fursa zaidi kwa kampuni za kigeni nchini China.

“Tutaendelea kujenga mazingira ya biashara yenye soko huria, yanayofuata sheria na yenye hadhi ya kimataifa, na kutoa huduma bora kwa wawekezaji wa kigeni,” amesema.

Kwa upande wake Sukanto Tanoto amesema kuwa ana matumaini juu ya soko la China na matarajio ya maendeleo ya China, na ataendelea kupanua uwekezaji nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha