Rubani wa Marekani afariki baada ya kujiua kwa kuchoma moto ili kupinga Israel

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 27, 2024

Picha ya Aaron Bushnell, rubani mmoja wa Jeshi la anga la Marekani ambaye alijiua kwa kuchoma moto Februari 25, Mwaka 2024 nje ya Ubalozi wa Israel mjini Washington ili kupinga operesheni ya kijeshi ya nchi ya Kiyahudi huko Gaza.  (Picha kutoka: heavy.com)

Picha ya Aaron Bushnell, rubani mmoja wa Jeshi la anga la Marekani ambaye alijiua kwa kuchoma moto Februari 25, Mwaka 2024 nje ya Ubalozi wa Israel mjini Washington ili kupinga operesheni ya kijeshi ya nchi ya Kiyahudi huko Gaza. (Picha kutoka: heavy.com)

Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilisema Jumatatu kuwa, Rubani mmoja wa Jeshi la anga la Marekani ambaye alijiua kwa kuchoma moto siku ya Jumapili nje ya Ubalozi wa Israel mjini Washington ili kupinga operesheni ya kijeshi ya nchi ya Kiyahudi huko Gaza.

Msemaji wa Jeshi la anga Rose Riley alisema mtu huyo "alijeruhiwa vibaya na kufariki dunia jana usiku. Tutatoa habari zaidi saa 24 baada ya kumaliza kazi ya kuarifu jamaa yake."

Idara ya Huduma za Zima Moto na Dharura ya Matibabu ya D.C. (EMS) ilisema kwamba walipata simu kuhusu mtu mmoja alichomwa moto nje ya ubalozi kabla ya saa saba mchana za siku ya Jumapili za saa za huko na kukuta moto imezimwa.

Rubani huyo alikuwa akivaa sare za kijeshi, alirekodi shughuli yake ya kutoa mashitaka mbele ya ubalozi huo, ambapo alisema “Sitakuwa mshirikiwa uangamizaji wa kabila,” yaani anapinga operesheni ya kijeshi ya Israel huko Gaza.

"Kuikomboa Palestine," alipiga makelele makali huku akijimwagia majimaji kwa kuchoma moto akajiua na kuanguka chini.

Alipelekwa katika hospitali ya huko akiwa amejeruhiwa vibaya sana, Idara ya Huduma ya Zima Moto na Dharura ya Matibabu ya D.C. (EMS) walisema.

Rubani huyo amethibitishwa na Idara ya Polisi ya D.C. kuwa ni Aaron Bushnell mwenye umri wa miaka 25 wa San Antonio, Texas.

Tukio hilo limetokea wakati mgogoro kati ya Israel na Hamas utaingia mwezi wa tano, huku kukiwa na shinikizo linaloongezeka, ikiwa ni pamoja na shinikizo nchini Marekani, inayoitaka Israel kuacha operesheni ya kijeshi kwenye ardhi kusini mwa Gaza, ambako zaidi ya raia milioni 1 wa Palestina wanaishi huko sasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha