China kufanya mipango ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Mwaka 2024, 2025

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 28, 2024

Picha iliyopigwa Septemba 9, 2020 ikionyesha mandhari ya maghorofa marefu   kwenye eneo la kiini la biashara (CBD) mjini Beijing, China. (Xinhua/Chen Zhonghao)

Picha iliyopigwa Septemba 9, 2020 ikionyesha mandhari ya maghorofa marefu kwenye eneo la kiini la biashara (CBD) mjini Beijing, China. (Xinhua/Chen Zhonghao)

BEIJING - Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya China imezitaka serikali za mitaa kote nchini China siku ya Jumanne kufanya mipango ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Mwaka 2024 na 2025.

Wizara hiyo imetoa waraka ukizitaka serikali za mitaa kukadiria mahitaji ya nyumba kutokana na mabadiliko ya idadi ya watu, kupanga kwa njia ya kisayansi ugawaji wa ardhi na kutoa fedha kwa miradi ya ujenzi wa nyumba kwa kuendana na mahitaji ya makazi.

Mkakati kama huo umepitishwa ili kupata uwiano kati ya ugawaji na mahitaji na muundo mzuri wa soko la nyumba, na kuzuia kusuasua kwa kasi kwa sekta hiyo, wizara imesema.

Imesisitiza umuhimu wa kujenga nyumba za kutosha za bei nafuu na kukidhi mahitaji ya kupandishwa ngazi kwa ujenzi wa nyumba wakati wa kufanya mipango ya maendeleo ya ujenzi wa nyumba.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha