Rwanda kuwa mwenyeji wa ofisi ya kikanda ya taasisi ya kimataifa ya chanjo

(CRI Online) Februari 28, 2024

Wizara ya Afya ya Rwanda na Taasisi ya Kimataifa ya Chanjo (IVI) zimetangaza kuwa Rwanda inatarajiwa kuwa mwenyeji wa ofisi ya Kanda ya Afrika ya Taasisi ya Kimataifa ya Chanjo, iliyopangwa kufunguliwa mwaka huu.

Bodi ya Wadhamini ya IVI imeithibitisha Rwanda kuwa eneo lake katika kanda ya Afrika kwenye mkutano wake uliofanyika mwezi Februari, kufuatia tathmini ya kina ya mapendekezo kutoka nchi tano kuwa mwenyeji wa ofisi ya kanda.

Waziri wa Afya wa Rwanda Sabin Nsanzimana amesema, Rwanda kuwa mwenyeji wa ofisi ya IVI ya kanda ya Afrika, ni hatua nyingine muhimu kuelekea Afrika yenye kujiandaa na dharura za afya ya umma zinazoweza kutokea.

Amesema Rwanda iko tayari kuendeleza ushirikiano muhimu na Taasisi ya Kimataifa ya Chanjo (IVI) na kuanzisha ushirikiano sawa na huo katika siku zijazo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha