

Lugha Nyingine
Rais Mwinyi aondoa kodi kwenye sukari
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoa tozo ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye bidhaa ya sukari ili kuwaepusha wananchi na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kuelekea mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Dkt. Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko kuu la Jumbi na Soko la samaki la Malindi katika Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani humo Februari 26 katika ziara yake maalumu alipotembelea masoko na kusikiliza changamoto zao.
Aidha, Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi ili kuwasaidia wananchi wanyonge kuelekea mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa upande mwingine Rais Mwinyi ameisisitiza Taasisi ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Zanzibar (ZEEA) kuwawezesha wafanyabiashara wa soko la samaki Malindi kwa kuwapatia mitaji ili kuendeleza biashara zao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma