

Lugha Nyingine
TRC yazindua majaribio ya kwanza ya treni inayotumia nishati ya umeme
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limezindua majaribio yake ya kwanza rasmi ya treni ya kwanza inayotumia nishati ya umeme nchini humo kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Bw. Mobhare Matinyi amesema katika uzinduzi huo kuwa serikali inalenga kuziunganisha nchi jirani kwa reli ya SGR.
Treni hiyo mpya ya kielektroniki inategemewa kubadilisha maisha ya watu na namna ya kufanya biashara ikitoa usafiri wa haraka, salama na wa bei nafuu.
Treni yenye kwenda kwa kasi ya Kilomita 160 kwa saa itakuwa ya thamani kubwa kwa wasafiri na wafanyabiashara. TRC ilipokea vichwa vitatu vya treni inayotumia umeme na mabehewa 27 mapya ya abiria mwezi Disemba mwaka jana.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa amesema majaribio ya sehemu ya pili kati ya Morogoro na Makutopora yataanza mwezi ujao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma