Makamu Rais wa China akutana na mkuu wa WWF

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 29, 2024

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Kirsten Schuijt, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Dunia wa Mazingira (WWF), mjini Beijing, China, Februari 28, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Makamu Rais wa China Han Zheng akikutana na Kirsten Schuijt, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Dunia wa Mazingira (WWF), mjini Beijing, China, Februari 28, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

BEIJING - Makamu Rais wa China Han Zheng amekutana na Kirsten Schuijt, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Mfuko wa Mazingira Duniani (WWF) siku ya Jumatano, akitoa wito wa ushirikiano wa karibu ili kukabiliana na changamoto za dunia nzima katika uhifadhi wa ikolojia.

Han amesema serikali ya China imeanzisha kithabiti na kutekeleza dhana ya maendeleo ya kijani na imepata mafanikio makubwa katika kujenga China yenye kupendeza.

Amesema Shirika la Kimataifa la WWF ni shirika mashuhuri la kimataifa la ulinzi wa mazingira ya asili ambalo lilishirikiana na China katika ulinzi wa Panda katika miaka ya 1980 na kwamba tangu wakati huo, limetoa mchango wenye hamasa kwa uhifadhi wa ikolojia na maendeleo endelevu ya China.

Han ameongeza kuwa mazingira ya asili ni msingi wa maisha ya binadamu, ambayo ni vigumu kuyarejesha mara yanapoharibiwa. Amesema China inatilia maanani sana ulinzi wa mazingira ya asili, na ni mshiriki, mchangiaji na mfuatiliaji katika juhudi za kujenga ustaarabu wa kiikolojia wa kimataifa.

Amesema China iko tayari kufanya ushirikiano wa karibu na Shirika la Kimataifa la WWF ili kukabiliana kwa pamoja na changamoto za dunia nzima katika uhifadhi wa mazingira ya asili.

Kwa upande wake Schuijt amesifu sana mchango uliotolewa na China katika uhifadhi wa mazingira ya asili na usimamizi wa ikolojia ya dunia nzima. Amesema shirika hilo lingependa kuimarisha ushirikiano wake na China katika kulinda bayoanuwai duniani na kuhimiza maendeleo endelevu ya dunia nzima.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha