

Lugha Nyingine
China yapanua mtandao wa usafiri ili kuwezesha maendeleo ya hali ya juu
Picha hii iliyopigwa Desemba 4, 2023 ikionyesha sehemu ya Barabara Kuu ya Wuxi-Zhenping katika Wilaya ya Wuxi, mjini Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua/Huang Wei)
BEIJING - China imepata mafanikio makubwa katika kuboresha mtandao wake wa miundombinu ya usafiri na huduma za usafiri katika mwaka uliopita, Wizara ya Uchukuzi ya China imesema siku ya Jumatano ambapo thamani ya uwekezaji wa rasilimali zisizohamishika katika mfumo wa usafiri wa nchi hiyo ilifikia yuan trilioni 3.9 (kama dola bilioni 548.7 za Kimarekani) katika Mwaka 2023.
Reli za mwendokasi zenye jumla ya urefu wa kilomita 2,776 zilifunguliwa, na barabara kuu zenye urefu wa kilomita 7,000 zilijengwa au kupanuliwa mwaka jana, Li Xiaopeng, waziri wa uchukuzi wa China, ameuambia mkutano na waandishi wa habari.
Amesema China iliongeza au kuboresha njia za meli zenye urefu wa kilomita 1,000, na idadi ya viwanja vya ndege kwa ajili ya usafirishaji ilifikia 259 huku huduma za posta zimeweza kupatikana kwa vijiji vyote kote nchini.
Wakati huo huo, huduma za usafiri za China ziliendelea kuboreshwa mwaka jana kutokana na muundo wa usafiri ulioboreshwa, kwa mujibu wa Li.
Kiasi cha usafirishaji wa mizigo nchini humo kilipanda kwa asilimia 8.1 mwaka hadi mwaka na kufikia tani bilioni 54.75 mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.9 kutoka Mwaka 2019.
Amesema usafiri wa abiria nao ulirekodi ukuaji thabiti. Usafiri wa abiria kati ya mikoa nchini China uliongezeka kwa asilimia 30.9 mwaka hadi mwaka na kufikia safari bilioni 61.25 Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.8 kutoka Mwaka 2019.
Kampuni za usambazaji wa mizigo kote nchini China zilishughulikia vifurushi bilioni 132 Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.4 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Sekta ilipata mapato ya jumla ya yuan trilioni 1.2 katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.3 mwaka hadi mwaka, amesema Zhao Chongjiu, mkuu wa Shirika la Posta la Serikali ya China, kwenye mkutano na waandishi wa habari.
China pia imekuwa ikiimarisha ushirikiano wake na nchi za nje. Maendeleo ya kiwango cha juu ya muunganisho wa usafiri chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja yamesogezwa hatua kwa hatua, Li amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma