UNECA yaitaka Afrika kutumia mtaji wa asili ili kuharakisha mageuzi kuelekea uchumi wa kijani

(CRI Online) Februari 29, 2024

Naibu katibu mtendaji wa Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Afrika (UNECA) Bw. Antonio Pedro, amesema ni lazima Afrika itumie mtaji wake wa asili ili kuharakisha mageuzi ya uchumi wa kijani.

Bw. Pedro amesema Bara la Afrika likiwa linakabiliwa na mizigo na hatari nyingi kutokana na matukio na mifumo inayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi, linatakiwa kupitisha suluhu za ndani kwa changamoto zake za maendeleo katika mfumo wa kifedha wa kimataifa.

Akiongea nchini Zimbabwe kwenye mkutano wa 56 wa wiki moja wa UNECA wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi wa Afrika, Bw. Pedro amesema kuna fursa ya kipekee ya kubadilisha nchi za Afrika kikamilifu kuwa na uchumi jumuishi, wenye utoaji wa hewa chafu chache na rasilimali zenye ufanisi.

Amesema hili linaweza kufikiwa kwa kuchanganya ahadi za mazingira na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ahadi za kijamii na kiuchumi na kutokomeza au kupunguza umaskini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha