Marais Ruto na Museveni wakutana kuhusu kazi ya Raila Odinga katika Umoja wa Afrika

(CRI Online) Februari 29, 2024

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na mwenzake wa Kenya, William Ruto wameafikiana kumuunga mkono Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya na Kiongozi wa Muungano wa Vyama vya Upinzani wa Azimio la Umoja, Raila Odinga juu ya azma yake ya kuwania Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).

Maafikiano hayo yamefanyika Jumatatu katika mualiko maalum wa Rais Museveni, shambani kwake Kisozi nchini Uganda. Kabla ya tangazo la viongozi hao wawili, timu ya kampeni ya kutaka Bw Odinga kuwa mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ilikuwa imetua Uganda ili kumshawishi Rais Museveni kuiunga mkono Kenya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha