Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China yafanya mkutano kujadili ripoti ya kazi ya Serikali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 01, 2024

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) tarehe 29 Februari ilifanya mkutano kujadili rasimu ya “Ripoti ya Kazi ya Serikali” ambayo Baraza la Serikali la China litawasilisha kwenye Mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China ili ithibitishwe. Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping ameongeza mkutano huo.

Mkutano huo umesema kuwa, katika mwaka uliopita, katika wakati wa kukabiliwa na mazingira ya kimataifa yenye utatanishi zaidi na kazi ngumu kubwa ya mageuzi, maendeleo na kudumisha utulivu, China iliifanya kazi yake ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya UVIKO-19 ihamie kwenye kipindi tulivu, na uchumi wake umerejea kwenye hali ya mwelekeo mzuri wa kuendelea kuongezeka. Malengo makuu ya maendeleo ya uchumi na jamii ya mwaka mzima yametimizwa kwa mafanikio, maendeleo ya kiwango cha juu yamesukumwa mbele kwa hatua madhubuti, na kupiga hatua kithabiti kwa kujenga mambo ya kisasa ya nchi ya kijamaa.

Mwaka huu ni wa maadhimisho ya 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na ni mwaka muhimu kwa kutimiza malengo ya “Mpango wa 14 wa Miaka Mitano (2021-2025)” wa China.

Ili kufanya vizuri kazi za serikali za mwaka 2024, ni lazima kushikilia msimamo wa jumla wa kujipatia maendeleo ya kazi kukiwa kuhakikisha utulivu, kutekeleza kikamilifu dhana mpya ya maendeleo kwa pande zote na kwa usahihi, kuharakisha kuunda muundo mpya wa maendeleo, na kuweka mkazo katika kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu.

Mkutano huo umedhihirisha kuwa, ni lazima kuongeza uhai wa uchumi kwa vitendo halisi, kuzuia na kuondoa hatari, kuyafanya matarajio ya jamii yawe mazuri, kuimarisha na kuendeleza mwelekeo mzuri wa ufufukaji wa uchumi na ongezeko la uchumi, na kuleta ustawi zaidi kwa maisha ya watu.

Mkutano huo umeeleza kuwa, ni lazima kuongeza nguvu kiasi cha kufaa kwa kutoa sera ya mambo ya fedha inayoweza kuchachua hamasa, kuongeza sifa bora na ufanisi mzuri, na sera ya fedha inapaswa kuwa na unyumbufu, ya kulenga kwa usahihi na kupata ufanisi. Inabidi kuhimiza kwa juhudi kubwa ujenzi wa mfumo wa viwanda vya kisasa, na kuharakisha kuendeleza nguvu mpya ya maendeleo yenye sifa bora. China itaendeleza mageuzi kwa kina bila ya kuyumbayumba, kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na kuhimiza mafungamano ya miji na vijiji na uratibu wa maendeleo ya maeneo tofauti.

Mkutano huo umeeleza kuwa, China pia itasukuma mbele maendeleo ya kijani ya utoaji mdogo wa kaboni, kuimarisha na kuvumbuza usimamizi wa jamii, na kujitahidi kutimiza malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii katika mwaka huu mzima.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha