Hengqin ya China yasamehe ushuru wa forodha wa bidhaa nyingi kutoka Macao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 01, 2024

Picha hii iliyopigwa kwa droni Novemba 4, 2023 inaonyesha mandhari ya Kituo cha mambo ya fedha cha Kimataifa cha Hengqin huko Zhuhai, Mkoa wa Guangdong kusini mwa China. (Xinhua/Liu Dawei)

Picha hii iliyopigwa kwa droni Novemba 4, 2023 inaonyesha mandhari ya Kituo cha mambo ya fedha cha Kimataifa cha Hengqin huko Zhuhai, Mkoa wa Guangdong kusini mwa China. (Xinhua/Liu Dawei)

Kisiwa cha Hengqin cha Mji wa Zhuhai wa Mkoa wa Guangdong kilianza kutekeleza hatua mpya ya forodha siku ya Ijumaa ambayo inaruhusu kusamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa nyingi zinazosafirishwa huko kutoka kwa Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao (SAR).

Hatua hiyo mpya ilianza kufanya kazi usiku wa manane katika Eneo la Ushirikiano wa Kina la Guangdong-Macao huko Hengqin, Mji wa Zhuhai. Kisiwa hicho chenye ukubwa wa kilomita za mraba 106 kiko kati ya Macao na China bara.

Chini ya mfumo mpya, ushuru wa forodha wa bidhaa zinazoingia Hengqin kutoka Macao utasamehewa, wakati bidhaa zinazosafirishwa kutoka Hengqin hadi sehemu mbalimbali nchini China sasa zitatozwa ushuru wa kuingizwa, kama bidhaa hizo hazilingani na masharti ya kusamehewa kwa ushuru wa thamani ya nyongeza.

Sera zinazofanana za kusamehewa kwa ushuru pia zinafaa kwa mizigo na vifurushi vinavyoingia Hengqin kutoka Macao.

Sera hiyo mpya inachukuliwa kuwa ni mpango mkubwa wa kuongeza uzoefu wa kufuata "nchi moja, mifumo miwili" huko Macao na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa aina mbalimbali wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao wa China.

Li Weinong, mkurugenzi wa kamati ya usimamizi wa eneo la biashara huria ya Hengqin alisema, "Sera mpya itahimiza kwa ufanisi mzunguko wa bidhaa, watu, mitaji na upashanaji wa habari kati ya Hengqin na Macao, na kuunda nafasi mpya thamini kwa viwanda vipya na hali mpya ya shughuli katika Macao ".

Mnamo mwaka wa 2021, serikali kuu ya China iliamua kujenga Eneo la Ushirikiano wa Kina la Guangdong-Macao huko Hengqin na kukifanya kisiwa hicho kuwa sehemu mpya muhimu ya kuleta ongezeko la uchumi wa Macao.

Takwimu zilizotolewa na Idara ya takwimu ya Hengqin zimeonesha kuwa, hadi kufikia mwisho wa 2023, wakazi wa Macao wanaofanya kazi au wanaoishi katika kisiwa cha Hengqin wamefikia 11,500, wastani wa ongezeko la mwaka ni zaidi ya asilimia 70.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha