Chapa za China zaongoza kwa mauzo ya magari yanayotumia umeme nchini Israel katika miezi ya Januari-Februari, Mwaka 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 04, 2024

Wateja wakitazama gari aina ya Atto 3 la Kampuni ya Magari ya BYD kwenye duka moja huko Tel Aviv, Israel, Julai 17, 2023. (Xinhua/Chen Junqing)

Wateja wakitazama gari aina ya Atto 3 la Kampuni ya Magari ya BYD kwenye duka moja huko Tel Aviv, Israel, Julai 17, 2023. (Xinhua/Chen Junqing)

JERUSALEM – Kampuni ya magari ya BYD ya China imeongoza mauzo ya magari yanayotumia umeme nchini Israeli katika miezi miwili ya kwanza ya Mwaka 2024, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Waagizaji wa Magari la Israel siku ya Jumapili ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kampuni hiyo, inayouza aina tano za magari yanayotumia umeme nchini Israeli, iliuza magari 5,290 katika miezi ya Januari-Februari. Mwaka jana, BYD iliongoza kwa mauzo ya magari hayo nchini humo kwa kuuza magari 15,145.

BYD pia imechukua nafasi ya tatu kwenye orodha ya jumla ya mauzo ya magari nchini Israeli katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, ambayo inajumuisha magari yanayotumia umeme na petroli.

Kampuni ya Magari ya Geely, ambayo ni kampuni nyingine ya magari yanayotumia umeme wa China, imechukua nafasi ya pili katika mauzo ya magari yanayotumia umeme nchini Israeli kwa miezi hiyo miwili ya kwanza ya Mwaka 2024 kwa kuuza magari 1,626 ya jiometri C.

Kampuni ya tatu katika orodha hiyo ni kampuni ya magari ya MG ya China yenye makao yake makuu nchini Uingereza, ambayo imeuza magari jumla ya 1,376 ya aina tano katika miezi ya Januari-Februari.

Chapa za magari za China zimechukua asilimia 77.1 ya mauzo yote ya magari yanayotumia umeme nchini Israeli katika miezi ya Januari-Februari, huku magari 11,784 yakiuzwa kwa jumla, kama ilivyoonyeshwa na takwimu hizo.

Chapa za magari za China pia zimeongoza mauzo ya magari ya abiria yaliyoagizwa kutoka nje nchini Israeli, yakijumuisha magari yanayotumia petroli na umeme, huku magari 14,255 yakiwa yameuzwa. Jamhuri ya Korea na Japan zikichukua nafasi ya pili na ya tatu mtawalia katika mauzo ya magari nchini humo, katika kipindi cha miezi hiyo miwili.

Wateja wakitazama gari aina ya Atto 3 la Kampuni ya Magari ya BYD kwenye duka moja huko Tel Aviv, Israel, Julai 17, 2023. (Xinhua/Chen Junqing)

Wateja wakitazama gari aina ya Atto 3 la Kampuni ya Magari ya BYD kwenye duka moja huko Tel Aviv, Israel, Julai 17, 2023. (Xinhua/Chen Junqing)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha