Ukuaji wa kasi wa uchumi wa China wasema hapana kwa kinachoitwa "kufika kilele cha ukuaji"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 04, 2024

Katika miaka ya hivi karibuni, sehemu mbalimbali za China zimehamasisha “injini imara” za uvumbuzi, na kuharakisha uanzishaji na uendelezaji wa vichocheo vipya vya maendeleo.

Hata hivyo, kuna baadhi ya watu wa Marekani na nchi za Magharibi wanaovaa “miwani ya rangi” na kudai kuwa “ukuaji wa uchumi wa China ni dhaifu na unakosa msukumo” na “ustawi wa China unakaribia mwisho.”

Hoja kama hizo za “kufika kilele cha ukuaji” hazina mantiki kabisa. Zinapuuza ukweli wa kimsingi - uchumi wa China katika zama mpya umehama kutoka hatua ya kukua kwa kasi hadi hatua ya kukua kwa ubora wa hali ya juu, na njia ya maendeleo inabadilika kutoka kusukumwa na rasilimali za uzalishaji hadi kusukumwa na uvumbuzi.

Mnamo 2023, uzalishaji wa bidhaa za betri za nishati ya jua, magari yanayotumia nishati mpya na seti za jenereta (vifaa vya uzalishaji umeme) umeongezeka kwa 54.0%, 30.3% na 28.5% mtawalia. Nyuma ya ukuaji huo ni mchanganyiko wa soko kubwa na uwezo wa uzalishaji na ugavi wa bidhaa wa China, ambao unabeba uwezekano mkubwa wa kifursa.

Mwaka huo huo uzalishaji wa bidhaa za teknolojia za akili mnemba wa China kama vile roboti za kutoa huduma na vifaa vya uchapishaji wa 3D umeongezeka kwa asilimia 23.3 na asilimia 36.2, mtawalia. Ripoti kutoka Shirikisho la Roboti la Kimataifa inaonesha kuwa, ufungaji wa roboti wa China unachukua asilimia 52 ya ufungaji wa jumla wa Dunia.

Na mwaka huo ongezeko la thamani la tasnia ya uundaji wa vifaa ya China limeongezeka kwa asilimia 6.8 kuliko mwaka uliotangulia, likichangia karibu asilimia 50 ya ukuaji wa viwanda vyote juu ya kigezo.

Maendeleo katika tasnia hizi tatu yanaakisi mwelekeo wa mageuzi ya teknolojia ya hali ya juu, ya akili mnemba, na ya kijani ya viwanda vya China. Mageuzi hayo ya kasi yamesababisha ustawi mkubwa wa tasnia zinazoibukia na ukuaji endelevu wa vichocheo vipya vya uchumi.

Baada ya miaka zaidi ya kumi ya maendeleo ya kasi, idadi ya kampuni za tasnia za kimkakati zinazoibukia ya China imeendelea kuongezeka hatua kwa hatua. Hadi kufikia mwezi Septemba 2023, kampuni za tasnia za kimkakati zinazoibukia zimepita milioni 2.

Kama Naibu Mkurugenzi wa Taasisi Kuu ya Sayansi ya Jamii ya China Wang Changlin alivyosema, baada ya mwaka 2023, maendeleo ya viwanda vya kimkakati vinavyoibukia vya China yamebadilika kutoka fanikio moja moja hadi mafanikio ya jumla kwa pande zote, yakiwa nguzo muhimu inayounga mkono ukuaji wa Uchumi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha