China yatimiza malengo makuu ya mwaka 2023

(CRI Online) Machi 05, 2024

The opening meeting of the second session of the 14th National People's Congress (NPC) is held at the Great Hall of the People in Beijing, capital of China, March 5, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Kikao cha ufunguzi cha mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China Machi 5, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

China imetimiza malengo na majukumu yake makuu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya mwaka 2023, licha ya matatizo na changamoto nyingi kutoka ndani na nje ya nchi, ripoti ya kazi ya serikali iliyowasilishwa Jumanne kwenye kikao cha mkutano wa Bunge la Umma la China kwa ajili ya kujadiliwa imesema.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo katika kipindi hicho pato la taifa la China liliongezeka kwa asilimia 5.2, likiifanya China kuwa moja ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi duniani.

Katika mwaka huo nafasi za ajira milioni 12.44 ziliundwa mijini, na wastani wa kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kilikuwa asilimia 5.2. Fahirisi ya bei ya walaji iliongezeka kwa asilimia 0.2, na usawa wa kimsingi ulidumishwa katika uwiano wa malipo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha