China yafungua "mikutano mikuu miwili" ya mwaka kudhamiria kuimarisha uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2024

Kikao cha ufunguzi wa mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) kikifanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing China, Machi 4, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)

BEIJING - "Mikutano Mikuu Miwili ya Mwaka" ya China, ambayo ni tukio ambalo husubiriwa kwa hamu kubwa kwenye kalenda ya kisiasa ya China, limeanza jana Jumatatu na leo Jumanne kutokana na kufunguliwa kwa mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) na mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, mtawalia huku ikibeba umuhimu mkubwa kwa China na kwingineko duniani.

Wakati nchi ya China ambayo ni ya pili kwa ukubwa wa uchumi wake duniani ikifanya juhudi za kuimarisha mwelekeo wa ufufukaji wa uchumi katika mchakato wa kufikia maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa, mikutano hiyo mwili ina umuhimu mkubwa kwa China na duniani kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya CPPCC Wang Huning alipotoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano uliohudhuriwa na viongozi wakuu wa chama na serikali wakiongozwa na Xi Jinping, alitoa ripoti ya kazi kwenye mkutano huo, akisema Mwaka 2024 CPPCC itaweka mkazo zaidi katika kusukuma mbele maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, kutoa maoni na mapendekezo na kuongeza maelewano mapana.

Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) wakifanyiwa mahojiano kabla ya ufunguzi wa mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya CPPCC kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing mjini Beijing, China, Machi 4, 2024. (Xinhua/Wang Jianhua)

Tukio kubwa la kisiasa

"Mikutano Mikuu Miwili" ni mikutano miwili ya mwaka ya Bunge la Umma la China na Kamati ya Kitaifa ya CPPCC.

Bunge la Umma la China lina mamlaka ya juu zaidi ya nchi ya kukagua ripoti ya kazi ya serikali, ambayo inaangazia mafanikio yaliyopita na kuweka malengo ya maendeleo kwa mwaka huu na kuendelea.

Zaidi ya yote, wajumbe wa bunge la umma la China na wale wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China wanafanya kazi muhimu sana katika kusukuma mbele maendeleo ya China.

Mwaka muhimu

"Mikutano Mikuu Miwili" ya mwaka huu ina umuhimu maalum kwani Mwaka 2024 ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na ni mwaka muhimu wa kufikia malengo na majukumu yaliyowekwa kwenye Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Miaka Mitano (2021-2025).

Uchumi wa China uliimarika Mwaka 2023, na kuonyesha maendeleo thabiti katika maendeleo yenye ubora wa hali ya juu. Pato la Taifa la China lilikua kwa asilimia 5.2 na kuzidi lengo la mwanzo la asiilimia 5.

Ingawa changamoto na matatizo bado yanaendelea kuwepo katika kuendelea kuhimiza ufufukaji wa uchumi wa China, lakini mwelekeo wa jumla wa uimarikaji na uboreshaji wa muda mrefu bado haujabadilika.

Picha hii iliyopigwa Februari 28, 2024 ikionyesha mikono ya roboti za viwandani zikifanya kazi kwenye karakana ya teknolojia za akili mnemba ya Wuxi, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Xinhua/Ji Chunpeng)

Maendeleo yenye ubora wa hali ya juu

Matarajio yanalenga kuona jinsi "mikutano mikuu miwili" itatilia maanani kuhimiza maendeleo yenye ubora wa hali ya juu, hayo ni matakwa muhimu kwa maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Wajumbe wa Bunge la Umma la China na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya CPPCC wana hamu ya kutoa maoni na mapendekezo kuhusu "nguvukazi yenye sifa mpya " ambayo imesisitizwa katika upangaji wa kazi za kiuchumi wa serikali kuu na za serikali za mitaa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha