Rais Xi Jinping asisitiza kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2024

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika  majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China. NPC) mjini Beijing, China, Machi 5, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuunda nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora zinazoendana na hali halisi ya China wakati wa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China aliposhiriki katika majadiliano ya wajumbe wa Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China siku ya Jumanne.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa wito kwa kutilia maanani maendeleo yenye ubora wa hali ya juu kama kipaumbele cha kwanza, akihimiza juhudi za kuongeza uvumbuzi, kuendeleza viwanda vinavyoibukia, kupitisha mipango yenye muono wa mbali ya kuendeleza viwanda vyenye mwelekeo wa siku za baadaye na kuboresha mfumo wa kisasa wa viwanda.

Kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora haimaanishi kupuuza au kuacha viwanda vya jadi, Rais Xi amesema. Ni muhimu kuzuia kukimbilia kwa kasi katika miradi na kuleta ongezeko la bei kwa viwanda, na kuepuka kutumia mtindo mmoja tu wa maendeleo, ameeleza.

Serikali za mitaa zinapaswa kufuata hali halisi ya rasilimali zao, msingi wa viwanda na hali ya utafiti wa kisayansi katika kuendeleza maendeleo ya viwanda vipya, miundo na vichocheo vya ukuaji wa uchumi kwa njia ya mpangilio mzuri, na kutumia teknolojia mpya kuzifanyia mageuzi na kuziboresha sekta za jadi kuwa viwanda vyenye kutumia teknolojia ya hali ya juu, akili mnemba na vya kijani, amesema.

Rais Xi alipojadili pamoja na wajumbe kuhusu ripoti ya kazi ya serikali alisifu maendeleo mapya ambayo Jiangsu imepata katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kuhimiza mkoa huo kuimarisha hali ya kujiamini na kujitokeza kwa pande zote kutoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Amesema ili kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora , mkoa wa Jiangsu lazima utilie maanani maendeleo ya mfumo wa kisasa wa viwanda huku viwanda vya teknolojia ya hali ya juu vikiwa kama uti wa mgongo, na kuharakisha juhudi za kuunda makundi ya viwanda vinavyoibukia vya kimkakati vyenye nguvu ya ushindani duniani.

Amehimiza kuufanya mkoa huo kuwa sehemu muhimu ya kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora katika uzalishaji wa viwanda mbalimbali. 

Rais Xi ametoa wito wa kupanga hatua kuu za kuimarisha zaidi mageuzi ya pande zote ili kuingiza msukumo mkubwa katika kuhimiza maendeleo yenye ubora wa hali ya juu na maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Ni muhimu kuharakisha uboreshaji wa taasisi za msingi katika maeneo kama vile ulinzi wa haki za kumiliki mali, ufikiaji wa soko, ushindani wenye haki na ufadhili wa kijamii ili kujenga mfumo wa hali ya juu wa uchumi wa soko wa kijamaa, amesema.

Kazi lazima ifanyike ili kuunga mkono ukuaji wa sekta binafsi na kampuni binafsi na kuchochea msukumo wa ndani na nguvu ya ubunifu wa mashirika mbalimbali ya biashara, Rais Xi amebainisha.

Pia amesisitiza kuimarisha mageuzi katika sayansi na teknolojia, elimu na mifumo ya usimamizi wa vipaji ili kuondoa matatizo na vikwazo kwa maendeleo ya nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora.

Ni muhimu pia kuhimiza uwekaji wa mazingira ya biashara ya kiwango cha kimataifa ambayo yanafuata mwelekeo wa soko, kufuata sheria na yenye ufanisi wa kimataifa, na kuunda nguvu mpya za uchumi wa kiwango cha juu wa kufungua mlango, amesema.

Rais Xi ametoa wito kwa Jiangsu kuunganishwa kikamilifu katika na kuchangia maendeleo ya Ukanda wa Kiuchumi wa Yangtze na maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Yangtze, na kuimarisha muunganisho na mikakati mingine ya maendeleo ya mikoa na mikakati mikuu ya kikanda.

Akihimiza Jiangsu kujenga minyororo mikubwa ya uvumbuzi, minyororo ya viwanda na minyororo ya ugavi, Rais Xi ameuagiza mkoa huo kuinua hadhi yake ya kuwa mkoa ulioendelea kiuchumi ili kuchochea na kushawishi maendeleo ya kimikoa na kitaifa.

Rais Xi pia ametoa wito wa kuendeleza juhudi za kuzidisha na kuimarisha msukumo wa kuimarika kwa uchumi ili kuongeza imani ya jamii nzima katika maendeleo.

Ameagiza hatua madhubuti za kurekebisha taratibu zisizo na maana na utendaji wenye urasimu. Amesema, hatua zenye matokeo halisi zinapaswa kuchukuliwa ili kupunguza mizigo kwa wale wanaofanya kazi chini, na kuchochea uwezo wa uvumbuzi ndani ya Chama na jamii nzima.

Rais Xi pia amesisitiza juhudi thabiti za kuimarisha ustawi wa watu huku kukiwa na maendeleo na kuhakikisha usalama mahali pa kazi.

Cai Qi, Mjumbe wa Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC, alishiriki katika mjadala huo. 

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika  majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China. NPC) mjini Beijing, Machi 5, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki katika  majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China. mjini Beijing, Machi 5, 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha