Uchaguzi nchini Sudan Kusini una hatari ya ghasia: Mkuu wa ujumbe wa kulinda amani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2024

UMOJA WA MATAIFA - Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Operesheni za Amani Jean-Pierre Lacroix Jumanne ameonya kwamba uchaguzi wa Sudan Kusini unakabiliwa na hatari ya ghasia na matokeo mabaya huku akisema uchaguzi lazima uchukuliwe kuwa wenye kuaminika na watu wa Sudan Kusini na unapaswa kuwa zoezi la kuunganisha watu badala ya kuwatenganisha.

Kuna maoni ya tofauti kati ya mirengo hasimu ya kisiasa katika maandalizi ya uchaguzi wa Desemba 2024 wa nchi hiyo. Mambo mengi yataathiri uchaguzi nchini Sudan Kusini, amesema.

Uchumi unaoibuka mpya umezidisha mapigano juu ya rasilimali na kusababisha ukosefu mkubwa wa ajira, haswa ukiathiri vijana. Aidha, ushindani wa kisiasa kati ya matabaka ya juu yanayotawala, umeongeza mapigano kati ya jamii tofauti na madhara ya ziada yanayosababishwa na wimbi la Wasudan Kusini wanaorejea nyumbani na wakimbizi wanaokimbia vita katika nchi jirani ya Sudan yote yameunganishwa kuelekea mambo yanayotathminiwa kuhusu uchaguzi huo, amesema.

"Kwa hivyo, kama havitashughulikiwa kwa uangalifu, vitakuwa na uwezekano wa vurugu na matokeo mabaya kwa nchi hiyo ambayo tayari ni dhaifu na kanda zima," amebainisha afisa huyo.

Umoja wa Mataifa unapaswa kusawazisha msimamo wake kuhusu masuala muhimu ya kisiasa nchini Sudan Kusini na IGAD na Umoja wa Afrika huku ukidumisha kutoegemea upande wowote na kujitegemea kwake. IGAD na Umoja wa Afrika zimetoa sauti ya kuunga mkono uchaguzi nchini Sudan Kusini na Umoja wa Mataifa, kwa hiyo, utatoa uungwaji mkono kadiri iwezekanavyo kwa mujibu wa mamlaka yake, amesema.

"Kushindwa kufanya hivyo siyo tu kunatishia hali ya kuaminika na utulivu unaotarajiwa wa uchaguzi, lakini pia makubaliano ya amani yenyewe," amebainisha.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha