Rais Xi atoa wito kwa washauri wa kisiasa kuzidisha maoni ya pamoja na kusaidia Ujenzi wa Mambo ya Kisasa ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2024

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akiwatembelea washauri wa kisiasa wa kitaifa kutoka Kamati ya Mapinduzi ya Kuomintang ya China, sekta ya sayansi na teknolojia, na sekta ya mazingira na rasilimali, wanaohudhuria mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing, China, Machi 6, 2024. (Picha na Sheng Jiapeng/Xinhua)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa washauri wa kisiasa wa China kuzidisha maoni ya pamoja na kusaidia ujenzi wa mambo ya kisasa ya China siku ya Jumatano, aliposhiriki katika mkutano wa pamoja wa kikundi kwenye mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amewataka washauri hao wa kisiasa kutoka pande tofauti za kisiasa, mashirika, makabila, sekta na nyanja zote za maisha wafanye utafiti wa kina na kufanya juhudi zaidi za kutoa maoni na mapendekezo kwa mujibu wa kazi kuu za kimkakati zilizowekwa na Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC na mipango iliyofanywa na Kamati Kuu ya CPC kuhusu Kazi ya Uchumi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na washauri wa kisiasa kutoka Kamati ya Mapinduzi ya Kuomintang ya China (RCCK), sekta ya sayansi na teknolojia, na sekta ya mazingira na rasilimali.

Rais Xi ametoa salamu za siku ya wanawake na kuwatakia kila kheri wanawake wa China wa makabila yote na kutoka nyanja mbalimbali wakati Siku ya Kimataifa ya Wanawake ya Tarehe 8 Machi inapowadia.

Wang Huning, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya CPPCC, na Cai Qi, Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC, walijumuika kwenye majadiliano. Wang na Cai wote ni wajumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.

Kwenye mkutano huo wa pamoja wa kikundi, washauri wa kisiasa sita wa kitaifa walizungumzia juu ya mada mbalimbali kuanzia zile za ushirikiano wa kuvuka Mlango-Bahari wa Taiwan katika minyororo ya viwanda na minyororo ya utoaji bidhaa hadi teknolojia kuu za intaneti na ulinzi wa mazingira.

Baada ya kuwasikiliza kwa makini washauri hao wa kisiasa, Rais Xi alitoa hotuba muhimu. Amesema Kamati Kuu ya CPC iliungana na kukiongoza Chama kizima na wananchi wa makabila yote kutimiza malengo makuu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii Mwaka 2023, ambapo washauri wa kisiasa wamechangia juhudi na hekima zao katika mafanikio hayo yaliyopatikana kwa bidii.

Kuhusu kazi inayohusiana na Taiwan, Rais Xi ameitaka Kamati ya Mapinduzi ya Kuomintang ya China kuuunganisha wazalendo wote wa ndani na nje ya China, ndani na nje ya Taiwan ili kuongeza juhudi za kupinga "kujitenga kwa Taiwan," kupanua uungaji mkono wa Muungano wa Taifa, na kuhimiza kwa pamoja mchakato wa Muungano wa Taifa wa amani.

Ametoa wito kwa juhudi kubwa za kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya pande mbili za Mlango-bahari katika maendeleo ya sekta za sayansi, kilimo, utamaduni na maendeleo ya vijana na kuimarisha maendeleo ya mafungamano ya pande mbili za Mlango-Bahari

Rais Xi amedhihirisha kuwa, washauri wa kisiasa na watu wote katika sekta ya sayansi na teknolojia wanatakiwa kuimarisha utafiti wa kimsingi na kutumia utafiti wa kimsingi, kufanya juhudi za kufikia mafanikio katika teknolojia kuu katika nyanja muhimu, na kuandaa vichocheo vipya vya kuendeleza nguvukazi mpya zenye sifa bora.

Rais Xi amewataka washauri wa kisiasa wa sekta ya mazingira na rasilimali kutoa mchango mpya katika ulinzi wa mazingira ya kiikolojia na kulinda kwa kiwango cha juu na kuwa tegemezi kwa maendeleo yenye ubora wa hali ya juu. Ametoa wito wa kutekeleza kikamilifu na kwa usahihi miongozo ya udhibiti wa uchafuzi wa mazingira unaolengwa, kuondoa uchafuzi kwa njia ya kisayansi na kwa mujibu wa sheria, kuendeleza maendeleo ya uchumi na jamii ya kijani na kutoa kaboni chache, na kufanya juhudi kubwa na kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya kuhimiza kufikia kilele cha utoaji wa kaboni na usawazishaji wa kaboni.

Rais Xi ameeleza kuwa, mwaka huu ni maadhmisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa CPPCC, vyombo vya mashauriano ya kisiasa vinatakiwa kuimarisha ujenzi wa utaratibu wa vyombo na ujenzi wa vyombo vyenywe, na kuwataka washauri wa kisiasa kuongeza sifa yao wenyewe na uwezo wao wa kutekeleza majukumu yao ili kuanzisha hali mpya ya kazi ya mashauriano ya kisasa na mambo ya ushirikiano wa vyama vingi chini ya uongozi wa Chama cha CPC.

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akiwatembelea washauri wa kisiasa wa kitaifa kutoka Kamati ya Mapinduzi ya Kuomintang ya China, sekta ya sayansi na teknolojia, na sekta ya mazingira na rasilimali, wanaohudhuria mkutano wa pili wa Kamati ya Kitaifa ya 14 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la Umma la China (CPPCC) mjini Beijing, China, Machi 6, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha