China itaendelea kuunga mkono kazi za UNRWA huko Gaza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2024

UMOJA WA MATAIFA - Geng Shuang, naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa, amesema kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne kwamba China itaendelea kuunga mkono kazi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) huko Gaza.

"China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuunga mkono kazi ya UNRWA na mashirika mengine ya kibinadamu huko Gaza na kufanya juhudi ili kumaliza uhasama huko Gaza, kupunguza majanga ya kibinadamu, kutekeleza suluhu ya kuunda mataifa mawili, na kufikia amani na utulivu wa kudumu katika Mashariki ya Kati," Geng amesema kwenye mkutano huo uliojikita katika kujadili suala la UNRWA.

Geng amesisitiza kuwa uwepo na kazi ya UNRWA imekuwa na umuhimu mkubwa na isiyoweza kuwa na mbadala kwa watu zaidi ya milioni 2 huko Gaza kupokea msaada wa kimataifa wa kibinadamu.

"Wakikabili tishio la maisha yao, wafanyakazi wa UNRWA wamejenga mstari wa maisha kwa watu wa Gaza kupitia juhudi zao na kujitolea kwao," amesema.

Geng Shuang amesema kuwa inasikitisha kwamba hivi karibuni UNRWA imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi na shutuma mfululizo zilizoratibiwa pamoja na kususiwa kwa upande mmoja na kutendewa isivyo haki na Israel.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha