

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China asema China itakuwa nguvu thabiti ya amani, utulivu na maendeleo ya dunia
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kuhusu sera ya mambo ya nje na uhusiano wa nje wa China pembezoni mwa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing, China, Machi 7, 2024. (Xinhua/Cai Yang)
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi leo Alhamisi amefanya mkutano na wanahabari kando ya mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China.
Bw. Wang amesema kwa sasa mazingira ya dunia yanashuhudia mabadiliko makubwa, na jamii ya binadamu inakumbwa na changamoto nyingi.
Amesema huku China ikikabiliwa na mazingira magumu na tete ya kimataifa, itakuwa nguvu thabiti ya amani, utulivu na maendeleo ya dunia.
Amesema, kwenye ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Rais Xi Jinping alisema zama hii ni zama yenye changamoto na pia yenye fursa na kwamba China itasimama kwenye mstari sahihi wa historia na maendeleo ya ustaarabu wa binadamu. Itanyanyua bendera ya amani, maendeleo, ushirikiano na kunufaishana, kujitafutia maendeleo chini ya msingi wa kulinda kithabiti amani na maendeleo ya dunia. Italinda vizuri zaidi amani na maendeleo ya dunia huku ikitafuta maendeleo yake yenyewe.
Amesema, ripoti hiyo ilisisitiza kuwa Chama cha Kikomunisti cha China kinaboresha maisha ya wananchi wa China na kurejesha ustawi wa taifa la China, pia kinadhamiria kutafuta maendeleo ya binadamu na mshikamano wa dunia.
Amesema, hayo ndiyo majukumu na wajibu wa China, na pia ni ndoto na malengo ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma