

Lugha Nyingine
Wang Yi: Jumuiya ya kimataifa lazima ichukulie usimamishaji mapigano mara moja na kukomesha vita huko Gaza kama kipaumbele
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kuhusu sera ya mambo ya nje na uhusiano wa nje wa China pembezoni mwa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing, China, Machi 7, 2024. (Xinhua/Wang Yuguo)
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Alhamisi mjini Beijing pembezoni mwa mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema jumuiya ya kimataifa lazima ichukulie usimamishaji mapigano wa mara moja na kukomesha vita huko Gaza kama kipaumbele chake kikuu.
Amesema watu wa Gaza wana haki ya kuishi na kwamba China inaunga mkono Palestina kuwa nchi mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma