Rais Xi Jinping asisitiza kuimarisha mageuzi ili kuongeza kwa pande zote uwezo wa kimkakati katika maeneo yanayoibukia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2024

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihudhuria mkutano wa wajumbe wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China kwenye mkutano wa pili wa Bune la Umma la 14 la China mjini Beijing, Machi 7, 2024. Xi ametoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo. (Xinhua/Li Genge)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihudhuria mkutano wa wajumbe wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) na Jeshi la Polisi la China kwenye mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing, Machi 7, 2024. Xi ametoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo. (Xinhua/Li Genge)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Alhamisi alipohudhuria mkutano wa wajumbe wa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China na Jeshi la Polisi la China kwenye mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China mjini Beijing alitoa wito kwa vikosi vya jeshi kuunda hisia kali za utume, kuimarisha mageuzi na kuhimiza uvumbuzi, ili kuongeza kwa pande zote uwezo wa kimkakati katika maeneo mapya yanayoibukia.

Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesema uwezo wa kimkakati katika maeneo mapya yanayoibukia ni sehemu muhimu ya mfumo wa mikakati na uwezo wa nchi, na yana umuhimu mkubwa katika kujenga nchi kubwa yenye nguvu na kuendeleza ustawishaji wa taifa katika sekta zote kupitia ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.

Wajumbe sita kutoka katika majeshi hayo walizungumza kwenye mkutano huo juu ya mada kuanzia zile za uwezo wa kiulinzi katika nafasi ya mtandao na matumizi ya akili mnemba hadi uendelezaji na uwezo wa utumiaji wa vifaa vya mapigano visivyoendeshwa na binadamu.

Rais Xi amesema msukumo wa China katika kuharakisha maendeleo ya nguvukazi mpya yenye sifa bora umetoa fursa adimu kwa kazi ya kujenga uwezo wa kimkakati katika maeneo yanayoibukia.

Ametoa wito wa kuhimiza mafungamano ya nguvukazi mpya yenye sifa bora na uwezo mpya wa kupigana vita wenye ufanisi mkubwa ili viwe na mwingiliano na kuhimizana.

Rais Xi amehimiza juhudi za kupanga mpango wa jumla kuhusu maandalizi ya kijeshi kwenye bahari, ulinzi wa haki na maslahi ya baharini na maendeleo ya uchumi wa baharini.

Ametoa wito wa kuboresha mpangilio wa anga ili kuhimiza maendeleo ya mfumo wa anga wa China, na kujenga mfumo wa ulinzi wa nafasi ya mtandao ili kuongeza uwezo wa kulinda usalama wa mtandao wa nchi.

Ameeleza kuwa ni muhimu kuongeza uvumbuzi wa kujitegemea na uvumbuzi asilia, ili kuhamasisha vichocheo vya ukuaji wa nguvukazi mpya yenye sifa bora na uwezo mpya wa kupigana vita wenye sifa bora ya juu.

Amesisitiza haja ya kuangazia mageuzi katika maeneo yanayoibukia kama kipaumbele cha kuendeleza kwa kina mageuzi kwa pande zote, akitaka kuwepo kwa mazingira ya mfumo wa uvumbuzi wa kujiamulia na kujiimarisha, kufungulia mlango na kufanya mafungmano, na kuwa na hamasa ya hali ya juu.

Rais Xi amesema, ni muhimu kuendeleza kwa kina mageuzi ya mfumo wa viwanda vya sayansi na teknolojia vinavyohusiana na ulinzi wa nchi, kuboresha mpangilio wa viwanda hivyo, na kukamilisha mfumo wa uitikiaji wa kasi wa teknolojia ya kisasa.

Pia amehimiza juhudi za kujenga minyororo ya uvumbuzi, minyororo ya viwanda na minyororo ya thamani iliyoundwa maalum kwa kuedana na maendeleo ya maeneo yanayoibukia, na kufanya uvumbuzi na utafiti kwa ujasiri juu ya ujenzi na matumizi ya aina mpya za vikosi vya kupigana vita. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha