China haitaruhusu kamwe Taiwan kujitenga na nchi mama: Waziri wa Mambo ya Nje wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2024

BEIJING - Sera ya China juu ya suala la Taiwan iko wazi, ambayo ni kuendelea kujitahidi kutimiza muungano wa taifa kwa amani kwa dhati mkubwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema Alhamisi kwenye mkutano na waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China.

"Jambo la msingi pia liko wazi kabisa: Hatutakubali kamwe Taiwan kujitenga na nchi mama," Wang amesema.

Akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu hali ya Mlango Bahari wa Taiwan baada ya uchaguzi wa viongozi na wabunge katika eneo la Taiwan, Wang amesema uchaguzi huo ni uchaguzi wa serikali za mitaa ya China na matokeo yake hayatabadili ukweli kwamba Taiwan ni sehemu ya China, wala hayatabadilisha mwenendo wa kihistoria kwamba Taiwan itarudi katika nchi yake ya mama.

"Kutakuwa na picha ya pamoja ya jumuiya nzima ya kimataifa ambapo nchi wanachama wote wanashikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja. Ni suala la muda tu," amesema.

Akibainisha kuwa kanuni ya kuwepo kwa China moja imekuwa makubaliano katika jumuiya ya kimataifa, ameonya kwamba wale ambao bado wanashirikiana na kuunga mkono "Taiwan kujitenga na China" wanachezea mamlaka ya China na nchi hizo zinazoshikilia kudumisha uhusiano wa kiserikali na Taiwan ndio zinaingilia masuala ya ndani ya China.

Shughuli za kutafuta ufarakanishaji wa Taiwan ijitenge zinaendelea kuwa sababu kuu ya kuharibu amani na utulivu wa Mlango-Bahari wa Taiwan, amesema.

"Kadiri kanuni ya kuwepo kwa China moja inavyokuwa na nguvu, ndivyo uhakikisho wa amani katika Mlango Bahari utakavyokuwa mkubwa," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha