Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya von der Leyen apata uungaji mkono wa chama kikubwa zaidi cha kisiasa cha EU kwa muhula wa pili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2024

Rais wa Kamisheni ya Ulaya (EC) Ursula von der Leyen akizungumza mjini Bucharest, Romania, Machi 7, 2024. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)

Rais wa Kamisheni ya Ulaya (EC) Ursula von der Leyen akizungumza mjini Bucharest, Romania, Machi 7, 2024. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)

BUCHAREST - Rais wa sasa wa Kamisheni ya Ulaya (EC) Ursula von der Leyen ameteuliwa na Chama cha Watu wa Ulaya (EPP), chama kikubwa zaidi cha kisiasa katika Bunge la Ulaya kwa ajili ya kuwania tena nafasi hiyo kwa muhula wa pili.

EPP kimepiga kura siku ya Alhamisi kwenye mkutano wake mkuu wa siku mbili mjini Bucharest, Romania ili kuidhinisha uteuzi wa von der Leyen. Mkuu huyo wa EC amepata kura 400 kati ya kura halali 489 zilizopigwa na kuwa mgombea pekee aliyeongoza orodha ya EPP kwa ajili ya kushiriki uchaguzi ujao wa bunge la Ulaya mwezi Juni.

Kwenye hotuba yale iliyotolewa mapema Alhamisi, von der Leyen ameahidi amani, ustawi na usalama kwa watu wa Ulaya.

Rais wa Kamisheni ya Ulaya (EC) Ursula von der Leyen akipiga makofi mjini Bucharest, Romania, Machi 7, 2024. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)

Rais wa Kamisheni ya Ulaya (EC) Ursula von der Leyen akipiga makofi mjini Bucharest, Romania, Machi 7, 2024. (Picha na Cristian Cristel/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha