Tume ya Wenyeviti ya mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la China  yafanya mkutano wake wa pili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 09, 2024

Zhao Leji, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Wenyeviti ya  mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, akiongoza mkutano wa pili wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 8, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

BEIJING – Tume ya Wenyeviti ya mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, imefanya mkutano wake wa pili siku Ijumaa ambapo Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa tume hiyo, aliongoza mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine uliamua kuwasilisha nyaraka mbalimbali kwa wajumbe ili kujadiliwa na kupitishwa.

Nyaraka hizo ni pamoja na mswada wa azimio la ripoti ya kazi ya serikali, mswada wa mpango wa kitaifa wa maendeleo ya uchumi na jamii wa Mwaka 2024, na mswada wa bajeti ya serikali kuu na za serikali za mitaa na bajeti za Mwaka 2024.

Nyaraka hizo pia zinajumuisha marekebisho ya mswada wa Sheria ya kimsingi kuhusu muundo wa vyombo na utaratibu wa kazi wa Baraza la Serikali la China.

Wenyeviti wa tume hiyo walikutana kabla ya mkutano huo ili kuandaa nyaraka.

Mkutano huo wa Tume ya Wenyeviti uliongozwa na Zhao, ambaye pia ni mwenyekiti wa Bunge la Umma la China.

Zhao Leji, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Wenyeviti ya  mkutano wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, akiongoza mkutano wa pili wa tume hiyo  kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 8, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha