

Lugha Nyingine
Bunge la Umma, Mahakama kuu ya umma ya China vyaapa kufanya kazi yenye sifa bora kuhimiza maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa
BEIJING – Vyombo vya Bunge la Umma la China, Mahakama Kuu ya Umma ya China (SPC), na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China (SPP) siku ya Ijumaa wakati wajumbe wakisikiliza ripoti za kazi zao kwenye kikao cha wajumbe wote kilichofanyika wakati wa mkutano mkuu wa pili wa mwaka wa Bunge la Umma la China, vimeahidi kuhimiza maendeleo ya kazi zao zenye sifa bora kwa hatua madhubuti katika Mwaka 2024 ili kusaidia ujenzi wa mambo ya kisasa ya China.
Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa China Xi Jinping, Li Qiang, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi, na Han Zheng.
Zhao Leji, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China, aliwasilisha ripoti ya kazi ya bunge kwenye kikao hicho.
Akikumbuka Mwaka 2023, Zhao amesema Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China NPC imetilia maanani kuongeza ubora wa utungaji wa sheria. Imethibitisha sheria 34 zilizotungw, na kupitisha sheria 21 kati yake, zikiwemo sheria sita mpya, sheria nane zilizofanyiwa marekebisho, na maamuzi saba kuhusu masuala ya kisheria na mambo makuu.
Kwa Mwaka 2024, Zhao amesema bunge la umma litachukua hatua madhubuti kwa kusukuma mbele maendeleo yenye sifa bora ya kazi ya Bunge la umma la China ili kutoa uhakikisho wa utekelezaji wa sheria kwa ajili ya kuhimiza kwa pande zote ujenzi wa mambo ya kisasa na ujenzi wa nchi yenye nguvu, pamoja na ustawishaji wa Taifa la China.
Bunge la Umma la China litaimarisha utekelezaji wa Katiba ya Nchi na usimamizi wa ufuataji wa katiba ya nchi, kukamilisha mfumo wa sheria wa ujamaa wenye umaalum wa China, na kuchukua hatua madhubuti za kufanya kazi ya usimamizi wenye ufanisi, na kuonesha vya kutosha umuhimu wa wajumbe wa bunge la umma, amesema.
Pia Bunge la Umma la China litaendeleza kwa kina mawasiliano na nje, na kuinua kiwango cha kazi ya kamati ya kudumu yenyewe ya bunge la umma.
Akitoa ripoti ya kazi ya mahakama kuu ya umma ya China, mkuu wa mahakama hiyo Zhang Jun amesema mahakama za China katika ngazi zote zilipokea kesi milioni 45.57 na kuhitimisha kesi milioni 45.27 Mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.6 na asilimia 13.4 kuliko mwaka 2022.
Katika mwaka uliopita, mahakama hiyo ilijikita katika msingi wa kutopendelea upande wowote na ufanisi katika kuendeleza kazi yake, Zhang amesema.
Amesema katika Mwaka 2024, mahakama kote nchini zitaelekeza kazi yao katika kuhimiza maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, kuharakisha kazi ya kuzifanya mahakama kuwa za kisasa, na kuboresha mfumo wa usimamizi.
Wakati akitoa ripoti ya kazi ya Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China, Mwendesha Mashtaka Mkuu Ying Yong amesema idara hiyo ikifuata wajibu wao wa usimamizi wa kisheria na kufanya kazi kwa sifa bora ili kila kesi ishughulikiwe kwa ufanisi na kwa sifa bora katika Mwaka 2023.
Ying amesema, idara za uendeshaji mashtaka kote nchini China zilishughulikia kesi milioni 4.25 Mwaka 2023, ambazo zimefikia ongezeko la asilimia 28.9 kuliko mwaka 2022.
Ametoa wito kwa waendesha mashtaka kote nchini China kuunga mkono ujenzi wa mambo ya kisasa ya China kwa kupitia kuzifanya kazi za uendeshaji mashtaka kuwa za kisasa, kulinda kwa uthabiti usalama wa nchi , utulivu wa jamii na ustawi wa watu, na kutoa huduma za kisheria kwa maendeleo yenye ubora wa hali ya juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma