Huduma za treni za mizigo za China-Ulaya zashuhudia upanuzi thabiti katika miezi miwili ya kwanza ya Mwaka 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 11, 2024

Treni ya mizigo inayotoa huduma kati ya China na Ulaya ikijiandaa kuondoka kutoka Bandari ya Horgos huko Horgos, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, Kaskazini-Magharibi mwa China, Januari 16, 2024. (Picha na Qiu Jing/Xinhua)

BEIJING – Takwimu zilizotolewa na Kampuni ya Reli ya China zimeonesha kuwa, huduma za treni za mizigo kati ya China na Ulaya zimerekodi upanuzi thabiti mnamo Januari na Februari mwaka huu, huku safari za treni za mizigo zinazotoa huduma kati ya China na Ulaya zikiwa zimefikia 2,928 katika miezi hiyo miwili ya kwanza ya Mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 9 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana.

Kontena 317,000 hivi za ukubwa wa futi ishirini zenye bidhaa zilisafirishwa kupitia huduma za treni hizo za mizigo katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10 kutoka mwaka wa 2023, shirika hilo limesema.

Kampuni hiyo imesema, hadi kufikia mwisho wa mwezi wa Februari, huduma hizo za treni za mizigo zilikuwa zimepanuka hadi kufikia miji 219 katika nchi 25 za Ulaya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha