Lugha Nyingine
Bara la Afrika laweka matumaini kwa jumuiya za washauri bingwa wa China na Afrika ili kuendeleza kasi ya ukuaji wa uchumi
Mshiriki akihudhuria Mkutano wa 13 wa Jukwaa la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika jijini Dar es Salaam, Tanzania, Machi 8, 2024. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)
DAR ES SALAAM - Mkutano wa 13 wa Jukwaa la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika umefunguliwa katika mji wa bandari wa Dar es Salaam, Tanzania siku ya Ijumaa, huku washiriki wakiueleza kuwa ni chachu kwa ajili ya kuendeleza ajenda ya uchumi na maendeleo ya viwanda ya Bara la Afrika.
James Mdoe, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania, amesema mkutano huo umeanzisha mazingira yenye hamasa katika nyanja ya taaluma na kwenye jamii kwa ajili ya kuimarisha uhusiano kati ya Afrika na China.
Akifungua mkutano huo wa siku moja, Mdoe amesema China na Afrika zinapaswa kutafuta namna ya kuzidisha ushirikiano na kufanya juhudi za kuonyesha mchango muhimu wa kimsingi ambao elimu inaweza kutoa katika kujenga jamii yenye nguvu kubwa.
Nelson Boniface, naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ametoa wito wa kuongezwa kwa ushirikiano kati ya China na Tanzania katika miradi ya kitaaluma na utafiti katika sekta za sayansi, elimu, sayansi ya jamii ya utamaduni, uhandisi na teknolojia ili kufikia mahitaji ya pande hizo mbili.
Chen Mingjian, Balozi wa China nchini Tanzania, amesema China na Afrika zina matarajio ya pamoja ya kutafuta njia za maendeleo kwa kujitegemea na kujenga pamoja jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja kwenye kiwango cha juu.
Mshiriki akihudhuria Mkutano wa 13 wa Jukwaa la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika jijini Dar es Salaam, Tanzania, Machi 8, 2024. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)
Mshiriki akihudhuria Mkutano wa 13 wa Jukwaa la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika jijini Dar es Salaam, Tanzania, Machi 8, 2024. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma