Huawei yafanya mashindano ya TEHAMA nchini Tunisia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 11, 2024

Waziri wa Teknolojia za Mawasiliano wa Tunisia Nizar Ben Neji akizungumza katika hafla ya kutunuku washindi ya Fainali ya Mashindano ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya Huawei Kanda ya Kaskazini mwa Afrika Mwaka 2023-2024 mjini Tunis, Tunisia, Machi 8, 2024. (Xinhua)

TUNIS - Fainali ya Mashindano ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya Huawei Kanda ya Kaskazini mwa Afrika Mwaka 2023-2024 imehitimishwa siku ya Ijumaa nchini Tunisia, huku timu 30 kutoka nchi tisa zimeshiriki.

Walimu na wanafunzi zaidi ya 100 wa vyuo vikuu kutoka nchi tisa za Afrika ambazo ni Tunisia, Algeria, Morocco, Ethiopia, Senegal, Libya, Misri, Cameroon na Mali, waliunda timu 30 kushiriki kwenye mashindano hayo. Timu zilizoibuka washindi katika mashindano hayo ya kikanda zitashiriki fainali nchini China mwaka huu.

Tukio hili limeonyesha uwezo wa Huawei na mchango wake katika maendeleo ya teknolojia ya Tunisia, pamoja na eneo zima la Afrika, Waziri wa Teknolojia za Mawasiliano wa Tunisia Nizar Ben Neji amesema katika hafla hiyo.

Thamani ya ushirikiano, ubora na uvumbuzi unaoakisiwa katika mashindano haya ni muhimu kwa uendelevu wa tasnia ya habari na mawasiliano, amesema Mohamed Ben Amor, katibu mkuu wa Shirika la TEHAMA la nchi za Kiarabu (AICTO).

Huawei imekuwa ikiunga mkono kikamilifu mkakati wa mageuzi ya kidijitali wa Tunisia, amesema Liang Feihu, mkurugenzi mkuu wa Huawei nchini Tunisia.

Liang ameongeza kuwa, Huawei imeanzisha ushirikiano wa kimkakati na vyuo vikuu na taasisi za utafiti zaidi ya 60 za Tunisia, na itafundisha watu 10,000 wenye ujuzi wa teknolojia za 5G, teknolojia ya wingu, na akili mnemba (AI) nchini Tunisia katika miaka mitano ijayo.

Mashindano hayo yameandaliwa na Kampuni ya Huawei nchini Tunisia kwa ushirikiano na Wizara ya Teknolojia za Mawasiliano ya Tunisia na Shirika la TEHAMA la nchi za Kiarabu (AICTO) na kufanyika kuanzia Machi 4 hadi 8. 

Washindi wa Fainali ya Mashindano ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya Huawei Kanda ya Kaskazini mwa Afrika Mwaka 2023-2024 wakiwa katika picha kwenye hafla ya kuwatunuku mjini Tunis, Tunisia, Machi 8, 2024. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha