

Lugha Nyingine
Chama tawala cha Rwanda cha RPF-Inkotanyi chamteua Paul Kagame kuwa mgombea urais
Chama tawala cha Rwanda, Rwanda Patriotic Front (RPF-Inkotanyi), kimemteua rasmi Rais aliye madarakani Paul Kagame kuwa mgombea wake wa urais kwa ajili ya uchaguzi ujao wa urais utakaofanyika mwezi Julai.
Rais Kagame ameteuliwa kwa kupata asilimia 99.1 ya kura zote halali zilizopigwa kwenye mkutano wa chama hicho, uliofanyika Jumamosi mjini Kigali.
Katika hotuba yake ya kukubali kuteuliwa, Rais Kagame ametoa shukrani kwa imani aliyopewa ya kuendelea kuijenga nchi. Pia amesisitiza umuhimu wa kuandaa viongozi wa kizazi kijacho ndani ya chama, akitaka wanachama kufikiria zaidi ya zama zao na kutilia maanani uongozi wa baadaye wa RPF-Inkotanyi.
Chama hicho pia kimetangaza orodha ya wagombea 70 wa ubunge na ilani yake ya uchaguzi itakayotekelezwa katika miaka mitano ijayo kama kitashinda uchaguzi. Mkutano wa chama hicho unafuatia chaguzi za mchujo za ndani ya vyama zilizofanyika mwezi Februari ili kuchagua watakaopeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi ujao wa rais na wabunge utakaofanyika Julai 15.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma