Safari za kitalii za raia wa kigeni nchini China kurahisishwa zaidi: Waziri wa Utalii wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2024

Watalii kutoka meli ya kitalii ya Zuiderdam wakitembelea eneo la kivutio huko Dalian, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China, Machi 10, 2024. (Xinhua/Pan Yulong)

Watalii kutoka meli ya kitalii ya Zuiderdam wakitembelea eneo la kivutio huko Dalian, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China, Machi 10, 2024. (Xinhua/Pan Yulong)

BEIJING - "Welcome to China!" Waziri wa Utalii na Utamaduni wa China Sun Yeli amesema kwa lugha ya Kiingereza siku ya Jumatatu alipokuwa akifafanua juu ya hatua za kurahisisha safari za kitalii za raia wa kigeni nchini China.

Sun ameangazia matatizo ya kulipa yanayowakumba watalii wanaosafiri nchini China kwani wanaona usumbufu wa kusafiri katika nchi hiyo ambapo malipo ya fedha kupitia simu janja imekuwa njia kuu ya malipo katika maeneo ya kibiashara kuanzia hotelini hadi maduka ya vyakula.

"Hakika hili ni tatizo lisilotarajiwa na la jipya kwani malipo kupitia simu za mkononi yanakua kwa kasi sana nchini China," Sun amewaambia waandishi wa habari kutoka ndani na nje ya China baada ya kufungwa kwa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China mjini Beijing.

Amesema mamlaka kuu zimekuwa zikifuatilia kwa ukaribu sana suala hili na zimeweka utaratibu wa uratibu ili kulitatua.

Hatua halisi zinatekelezwa, kama vile kuanzisha upya na kuboresha vifaa vya kuuza bidhaa, ili kuhakikisha kuwa watalii wa kigeni wanaposafiri nchini China, wataweza kutumia kadi za benki katika maeneo mbalimbali, kama vile hoteli, viwanja vya ndege, vivutio vya watalii na maduka. Wanaweza pia kuchagua kuskani msimbo wa QR au kutumia pesa taslimu kufanya malipo, Sun amesema.

Majukwaa ya malipo na kampuni za China zimefanya kazi pamoja ili kurahisisha mchakato wa watalii wa kigeni wanaoingia nchini China kujiandikisha kwa ajili ya malipo nchini China, na maeneo yote ya matumizi katika manunuzi yanalazimika kupokea fedha taslimu za China, Sun amesema.

"Tunaboresha kila hatua ya mchakato wa utalii wa ndani, kurahisisha taratibu kuanzia kuomba visa hadi upangaji wa safari wa ndege, kufanya taratibu za kujisajili hotelini, ununuzi wa bidhaa na kutembelea maeneo ya vivutio," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha