Soko la Magari yanayotumia Umeme la Uturuki lashuhudia ongezeko la magari kutoka China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 12, 2024

Magari yanayotumia umeme (EV) ya kampuni ya magari ya MG ya China yakioneshwa kwenye kituo cha mauzo cha MG huko Istanbul, Uturuki, Machi 4, 2024. (Picha na Safar Rajabov/Xinhua)

Magari yanayotumia umeme (EV) ya kampuni ya magari ya MG ya China yakioneshwa kwenye kituo cha mauzo cha MG huko Istanbul, Uturuki, Machi 4, 2024. (Picha na Safar Rajabov/Xinhua)

ISTANBUL - Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, soko la Uturuki limeshuhudia ongezeko la kasi la chapa za magari yanayotumia umeme kutoka China, ambayo yanavutia ufuatiliaji mkubwa zaidi zaidi wa wateja wa Uturuki.

Wataalamu wa sekta hii wanahusisha ongezeko hilo na mvuto wa magari yenye ubora wa juu, ufanisi wa hali ya juu na bei nafuu, pamoja na huduma za pande zote na matumizi yenye ufanisi ya nishati.

Tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Magari ya MG ya China nchini Uturuki Mwaka 2021, kampuni nyingine nyingi za China zilifuata mkondo huo haraka, na kufanya idadi ya jumla ya kampuni hizi kuwa 12 hadi Februari mwaka huu, kama ilivyobainishwa na Shirikisho la Wasambazaji na Usafirishaji wa Magari la Uturuki (ODMD) katika ripoti yake mpya ya mauzo.

Kiwango cha kutambuliwa kwa kampuni ya MG kiliongezeka hadi asilimia 79 mwaka jana, na kuifanya MG kuwa “chapa inayokua kwa kasi zaidi” nchini Uturuki, kwa mujibu wa ODMD.

Gari aina ya Atto 3 la Kampuni ya BYD na MG 4 la Kampuni ya MG, yote yakiwa ni magari yanayotumia umeme (EV) ya China, yameshika nafasi ya tatu na ya nne katika orodha ya magari yanayotumia umeme yaliyouzwa vizuri zaidi mwezi Februari nchini humo, kwa mujibu wa ODMD.

ODMD, moja ya mashirikisho makubwa ya sekta hii nchini Uturuki, lina wanachama 32 wanaowakilisha kampuni 52 za kimataifa hadi kufikia mwanzoni mwa 2024.

Semih Eryukseldi, mkongwe wa sekta ya mgari mwenye uzoefu wa karibu miaka 14 huko Istanbul, anasema ufuatiliaji wa wateja wa Uturuki kwa magari ya China unatokana na uwiano wa bei na ufanisi wa magari.

"Wateja wa Uturuki wamegundua kwamba wanaweza kununua magari yanayotumia umeme yenye vifaa vya kutosha, yenye ufanisi na ya bei nafuu," ameongeza.

Wafuatiliaji wa sekta ya magari nchini humo wanakadiria kuwa mgao wa bidhaa za China katika soko la Uturuki, ambao ulizidi asilimia 4.5 Mwaka 2023, huenda ukafikia asilimia 10 mwaka huu. 

Gari aina ya MG 4, ambalo ni gari linalotumia umeme (EV) lililotengenezwa na kampuni ya magari ya MG ya China, likiwa linachaji huko Istanbul, Uturuki, Machi 4, 2024. (Picha na Safar Rajabov/Xinhua)

Gari aina ya MG 4, ambalo ni gari linalotumia umeme (EV) lililotengenezwa na kampuni ya magari ya MG ya China, likiwa linachaji huko Istanbul, Uturuki, Machi 4, 2024. (Picha na Safar Rajabov/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha