Mwenyekiti wa Bunge la Umma la China akutana na wafanyakazi wa vyombo vya habari walioripoti habari za mkutano mkuu wa mwaka wa bunge hilo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2024

Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China akikutana na wafanyakazi wa vyombo vya habari walioripoti habari kuhusu mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China,  na ametoa salamu na shukrani zake  kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 11, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

BEIJING - Zhao Leji, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China amekutana na wafanyakazi wa vyombo vya habari walioripoti habari kuhusu mkutano mkuu wa pili wa Bunge la Umma la 14 la China, akitoa salamu na shukurani zake siku ya Jumatatu.

Zhao amesema, idara husika za serikali na vyombo vikuu vya habari vimetoa mchango mkubwa katika kuripoti habari na utangazaji wa mkutano huo mkuu wa bunge.

Akitoa rejelea kwa taarifa za habari mbalimbali za kina na za hamasa zilizoripotiwa na vyombo vya habari, Zhao amehimiza juhudi zaidi za kuunga mkono kuripoti habari na utangazaji wa mabunge ya umma na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Bunge la Umma la China.

Pia amesisitiza umuhimu wa kuangazia kwa uaminifu habari kuhusu mabunge ya umma, demokrasia na utawala wa kisheria nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha