Meli ya Kimataifa ya Kitalii inayobeba watalii zaidi ya 1,100 yawasili Tianjin ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2024

Picha iliyopigwa Machi 11, 2024 ikionyesha meli ya Zuiderdam, inayoendeshwa na Holland America Line, ikitia nanga kwenye Bandari ya Meli za Kimataifa za Kitalii ya Tianjin , Kaskazini mwa China. (Xinhua)

Picha iliyopigwa Machi 11, 2024 ikionyesha meli ya Zuiderdam, inayoendeshwa na Holland America Line, ikitia nanga kwenye Bandari ya Meli za Kimataifa za Kitalii ya Tianjin, Kaskazini mwa China. (Xinhua)

TIANJIN - Meli ya kitalii ya Zuiderdam, inayoendeshwa na kampuni ya Holland America Line, imetia nanga katika Bandari ya Meli za Kimataifa za Kitalii ya Tianjin, siku ya Jumatatu asubuhi, ikiwa na watalii zaidi ya 1,100 kutoka nchi na maeneo 30 ndani yake.

Hii inaashiria safari ya kwanza ya meli ya kitalii yenye urefu wa mita 285 na upana wa mita 32 katika mji huo wa Tianjin, ambapo itakaa kwa siku mbili na usiku mmoja. Abiria hao watatembelea vivutio katika miji ya Beijing, Tianjin na Xi'an.

Mfululizo wa hatua za huduma zilizopitishwa na idara ya forodha na shirika la meli za kitalii la mji huo zimewezesha safari hiyo ya meli mjini Tianjin.

Bi Linlin, ofisa ukaguzi wa uhamiaji wa mji huo, amesema walifanya kazi na shirika hilo la usafiri wa meli za kitalii na kampuni ya bandari hiyo ili kurahisisha taratibu za vibali vya abiria na kukidhi mahitaji ya watalii.

Ikiwa ni bandari kubwa zaidi ya watalii kaskazini mwa China, Bandari ya Meli za Kimataifa za Kitalii ya Tianjin imekaribisha meli 16 za kitalii na kushuhudia safari 50,000 za watalii hadi kufikia sasa mwaka huu, kwa mujibu wa Dong Zichen, naibu meneja mkuu wa kampuni inayoendesha bandari hiyo.

Tuna matumaini makubwa juu ya kuimarika kwa sekta ya utalii wa meli za kitalii mjini Tianjin," Dong amesema.

"Pamoja na sera za uungaji mkono za serikali na mahitaji ya watu kuongezeka kwa utalii wa meli, tunaamini kuwa sekta ya utalii wa meli itakua haraka nchini China," amesema Jiao Deshuai, meneja msaidizi mwandamizi wa idara ya usafiri wa meli katika Kampuni ya Kontena ya Sinotrans ya China Kaskazini, ambayo inajishughulisha na biashara ya wakala wa meli.

Baada ya kusafiri katika miji ya Shanghai na Dalian, meli hiyo ya Zuiderdam ilikuwa imeondoka Tianjin kuelekea Hong Kong jana Jumanne alasiri. 

Picha iliyopigwa Machi 11, 2024 ikionyesha meli ya Zuiderdam, inayoendeshwa na Holland America Line, ikitia nanga kwenye Bandari ya Meli za Kimataifa za Kitalii ya Tianjin, Kaskazini mwa China. (Xinhua)

Picha iliyopigwa Machi 11, 2024 ikionyesha meli ya Zuiderdam, inayoendeshwa na Holland America Line, ikitia nanga kwenye Bandari ya Meli za Kimataifa za Kitalii ya Tianjin, Kaskazini mwa China. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha