China yakamilisha ujenzi wa muundo wa jukwaa la kina kirefu baharini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2024

Picha iliyopigwa Machi 12, 2024, ikionyesha eneo la ujenzi wa muundo wa jukwaa la kina kirefu baharini la Haiji-2 katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Picha imetolewa na Shirika la Taifa la Uchimbaji Mafuta Baharini la China (CNOOC))

Picha iliyopigwa Machi 12, 2024, ikionyesha eneo la ujenzi wa muundo wa jukwaa la kina kirefu baharini la Haiji-2 katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Picha imetolewa na Shirika la Taifa la Uchimbaji Mafuta Baharini la China (CNOOC))

SHENZHEN - China imekamilisha ujenzi wa muundo wa jukwaa la kina kirefu baharini katika mkoa wa kusini wa Guangdong, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Taifa la Uchimbaji Mafuta Baharini la China (CNOOC) siku ya Jumanne ambapo jukwaa hilo la Haiji-2 lenye urefu wa mita 338.5 litafanya kazi kwenye wastani wa kina cha mita 324 na uzito wake ni tani 37,000, likivunja rekodi za Bara la Asia kwa urefu wake wa muundo, uzito, urefu wa kina litakachofanya kazi na kasi ya ujenzi.

Majukwaa ni miundo ambayo inawekwa chini ya bahari, yanayotumika kama msingi wa vifaa vya kuzalisha mafuta na gesi baharini.

Jukwaa hilo la Haiji-2 linatumia sahani mpya ya chuma iliyotengenezwa yenye nguvu kubwa ya megapascal 420 ambayo inachukuliwa kama muundo bunifu na wa mwepesi wenye gharama nafuu kwa majukwaa makubwa ya baharini, kwa mujibu wa Fu Dianfu anayefanya kazi katika taasisi ya utafiti ya CNOOC.

Jukwaa hilo linaonyesha uwezo wa China wa kujenga majukwaa ya kina kirefu baharini yaliyowekwa katika kina kirefu cha zaidi ya mita 300, amesema Wang Huoping, mhandisi katika shirika hilo tawi la Shenzhen.

Jukwaa la Haiji-2 linatarajiwa kufungwa hivi karibuni katika eneo la uchimbaji mafuta katika sehemu ya bahari ya Bonde la Pearl River Mouth.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha